Kama kuna gemu ambalo limechezwa sana na watoto na vijana wa miaka ya 90 basi ni ‘Brick Game’. Toleo la gemu hilo kwa ajili ya simu za Android na iPhones linapata umaarufu sana kwa sasa, na kama ulishachezaga gemu hili miaka ile ya nyuma basi unajua ni jinsi gani kupata nafasi ya kujikumbusha tena ni jambo la kuvutia na kufaraisha sana.
Magemu mengi yanayopata umaarufu siku hizi kwa watumiaji wa simu ni magemu yaliyoraisi kueleweka na pia yenye kuitaji ujanja kufanikiwa, na Brick Game ni moja wapo. Unachotakiwa kufanya ni kupanga matofali yanayokuja kwenye maumbo tofauti tofauti na kuhakikisha unavunja misingi kabla ya ukuta unaojengeka kufika juu. Watengenezaji wa gemu hili wamejitahidi sana katika kuhakikisha unaendelea kupata muonekano kama ule wa zamani.
Je wewe ulicheza gemu ili miaka ileee? Tuambie ilikuwa miaka gani? Kushusha gemu ili kwenye simu yako bofya -> Android | iOS
No Comment! Be the first one.