Wasomaji wetu wengi wa teknokona wamekuwa wakihitaji sana msaada wa kutaka kutumia akaunti mbilimbili za WhatsApp, Instagram, Facebook, Twitter, Snapchat, n.k katika simu moja.
Mbinu za kuwa na akaunti mbili kwa programu moja zipo nyingi na zina maelekezo tofauti. Wengi wamekuwa wakilazimika kuweka programu tofauti tofauti kufanikisha malengo hayo.

Aidha, wengine wamelazimika kuwa na simu zaidi ya moja ili kufanikisha kumiliki akaunti mbili za WhatsApp au Instagram ama Facebook. Leo tutakufahamisha kwa ufupi njia rahisi kufanya zoezi hilo la kuwa na programu aina moja kwa akaunti mbili.

Unachotakiwa kuwa na programu ambazo ushaziweka katika simu yako mfano WhatsApp, Instagram, Facebook, Twitter na pamoja na kuwa na progarmu hizo unaweza ukawa unahitaji kuwa na akaunti ya Instagram, Telegram na nyinginezo.
Unaweza kuamua ni programu ipi iwe mara mbili au la! Hatua za kufuata ni hizi zifuatazo:-
1. Ingia Play store andika Parallel space, ipakuwe kisha ihifadhi (install). Ukishamaliza ifungue utaona programu zote zilizo kwenye simu yako,
2. Weka tiki programu unazotaka ziwe mara mbili. Ukishamaliza kuweka tiki bonyeza sehemu iliyoandikwa ‘Add to Parallel Space‘.Utaziona programu zote unazotaka ziwe mara mbili. Utafungua yoyote kati ya hizo na kuanza kuitumia (mfano kama WhatsApp utafuata hatua zote za kusajili akaunti yako nyingine).
Kumbuka: Unaweza kuweka icon ya programu husika iwe kwenye shortcut kwa kuishikilia na kuiburuza mpaka kwenye neno shortcut.
Njia rahisi ni kuingia Play Store na kupakuwa app inayoitwa Parallel space, ina rangi tatu:- bluu, njano na nyekundu. Ukishaiweka programu hiyo itakuwezesha kuwa na programu ya pili ya kila uliyoweka katika simu yako.