fbpx

Kivinjari cha Samsung ni maarufu! Sasa kimepakuliwa zaidi ya mara bilioni 1

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +

ICT CONFERENCE 2019

Sambaza

Kivinjari cha Samsung (Samsung Internet Browser) katika takwimu za hivi karibuni zinaonesha kinazidi kupata umaarufu. Hii ni kutokana na kufikisha idadi ya kupakuliwa (Download) bilioni 1 katika soko la Play Store, hii ni kuliko vivinjari vya Firefox na Opera.

Kivinjari cha Samsung mara nyingi huja kikiwa kimewekwa kabisa katika simu za Samsung na kwa simu zingine za mfumo wa Android wanaweza kupakua katika Play Store.

Kivinjari cha Samsung

Data za Google PlayStore (Feb, 2019)

Kivinjari hicho ambacho kinasifika kwa wepesi na ubora mzuri, takwimu zinaonesha tangu mwezi Desemba kilishapakuliwa zaidi ya mara bilioni moja (1,000,000,000+), bado Opera na Firefox vipo katika idadi ya mamilioni 100 na zaidi.

INAYOHUSIANA  Kuharibika kwa Setilaiti ya Facebook, Tanzania na Afrika zimekosa Fursa?

Inawezekana Opera na Firefox havipo nyuma sana kwa kuwa Google wanaweka idadi ya kimafungu, yaani 1,000 na zaidi, 10,000 na zaidi, 100,000 na zaidi hivyo hivyo hadi kufika milioni 100 na zaidi, na kutoka hapo ndio inakuja bilioni na zaidi. Opera na Firefox kwa sasa wote wapo kwenye idadi ya milioni 100 na zaidi –  hii ina maanisha wapo kwenye idadi ya download milioni 100 hadi milioni 999.

samsung browser

App ya Samsung Browser

Kivinjari cha Samsung kinapatikana bure Play Store kwa simu za mfumo wa Android kuanzia toleo la lollipop 5.0 na kuendelea. Pia faida nyingine kwao kubwa kuleta idadi kubwa ni kutokana na kuja na simu zao za Samsung, ila inaonekana watumiaji wengi bado wanapendezwa nacho, ni kivinjari chenye kura nzuri za ubora kwenye Google PlayStore. Kina pointi 4.4 kati ya point 5.

INAYOHUSIANA  Sasa unaweza kuagiza chakula Facebook.

Kwa anayetaka kupakua na kuweka kwenye simu yake afungue link hapo chini.

Samsung Internet Browser

Facebook Comments

Sambaza

ICT CONFERENCE 2019

Share.

About Author

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.

Comments are closed.