fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

Google Google Pixels simu Teknolojia

Google Pixel 5a 5G itatoka mwaka huu

Google Pixel 5a 5G itatoka mwaka huu

Zilikuwepo habari za chini chini kuhusiana na mpango wa Pixel 5a 5G kutozinduliwa lakini habari hiyo imekanushwa vikali na Google wenyewe na ukweli ni kwamba itatoka mwaka huu.

Google imethibitisha kuwa moja ya simu janja zake itatoka mwaka huu na hii inafuatia taarifa kuwa Pixel 5a 5G ilikuwa imewekwa kando kutokana na sababu za kutokuwepo kwa vipuri mama vya kutosha kuwezesha kiwango kilichokusudiwa kuweza kutoka.

Zilikuwepo taarifa kutoka YouTube kuwa Google imesitisha mpango wa kutoa Pixel 5a lakini taarifa kwa mujibu wa taarifa rasmi kutoka kwa mzungumzaji wa kampuni amesema wao wahakusema kuwa watatoa toleo mbili tofauti kwa maana ya kwamba 5a na 5a 5G.

Kwa mujibu wa mzungumzaji huyo alisema mpango wa kutoa Pixel 5a 5G baadae mwaka huu upo palepale na zitapatikana kweneye masoko ya Japan na Marekani.

itatoka mwaka huu

Inayoaminika kuwa Pixel 5a 5G ambayo itatoka mwaka huu.

Mbali na hilo inaamnika kuwa Pixel 6 pia inaweza kuzinduliwa pamoja na Pixel 5a 5G ingawa Google wenyewe hawajasema chochote kuhusiana na hilo.

Mwaka jana Google walitoa Pixel 4a kwenye masoko ya Marekani na Japan mwezi Agosti hivyo inaaminika kuwa hata hii ijayo tuitegemee nyakati zilezile.

Je, wewe unatumia mojawapo ya toleo la simu janja za Pixel? Unaizungumziaje? Tupe maoni yako na daima usiache kutufuatilia kwa habari mbalimbali zinazohusu teknolojia.

Vyanzo: GSMArena, 9to5Google

SOMA PIA  Fununu Kuhusu Ujio Wa Huawei P9!
Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia.

Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania