fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

Apple Samsung simu Teknolojia Xiaomi

Simu janja za Apple kinara kwenye mauzo ya mwezi Januari

Simu janja za Apple kinara kwenye mauzo ya mwezi Januari

Kuna simu janja nyingi zipo sokoni na kila siku zinauzika kutokana na kile ambacho watu wanahitaji ili kuweza kubadilisha rununu moja kwenda nyingine. Simu janja za Apple zimekuwa kinara kwenye mauzo ya mwezi Januari; rununu 6/10 ni za Apple.

Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na Counterpoint ambao wanajulikana kwa kufanya tafiti za mauzo ya simu janja hivi karibu wametoa takwimu zilizoonyesha simu janja 10 zilizofanya vizuri zaidi kwenye mauzo ya soko kwa mwezi Januari tu; rununu 6 kati ya 10 ni za Apple na iPhone 12 ikiwa ndio kinara.

SOMA PIA  Aishtaki Apple, Asema Imeiba Ubunifu Wake Na Inabidi Imlipe Dola Bilioni 10 Kama Fidia!

Simu janja hizo 6/10 ni iPhone 12, iPhone 12 Pro Max, iPhone 12 Pro, iPhone 11, iPhone 12 Mini na iPhone SE 2020 ambazo zimewezesha Apple kupata 71% ya mauzo yote kwa mwezi Januari pekee. kampuni nyinginezo zilizofanya vizuri kimauzo ni Xiaomi na Samsung kwa bidhaa za Redmi 9A, Redmi 9, Samsung Galaxy A21s na Samsung Galaxy A31 ambazo ni sawa na zaidi ya 25% ya mauzo yote.

Simu janja za Apple

Simu janja 10 zilizofanya vizuri kimauzo mwezi Januari 2021.

Nini siri ya mafanikio ya Apple kimauzo?

Apple yenye makao yake makuu Cupertino, California-Marekani moja ya tatu (1/3) ya mauzo yake yanatoka nchini humo lakini pia mhitaji ya simu janja zenye teknolojia ya 5G ndani ya Marekani nayo ymechagiza mafanikio hayo ukizingatia toleo zote za iPhone 12 ni za 5G.

SOMA PIA  SONY Watangaza Play Station VR – Batman, Spiderman kuanza kutumika

iPhone 12 Mini yayo imetokea kwenye orodha za simu janja 10 bora zilizofanya vizuri kimauzo mwezi Januari 2021 lakini zipo taarifa zinazosema huenda Appple wakasitisha utengenezaji wa simu hizo kwenye robo ya pili ya mwaka huu.

Simu janja za Apple

iPhone 12 ambazo zite zina teknolojia ya 5G.

Ni wazi kwamba teknolojia ya 5G inazidi kupendwa na kwa ujio wa simu janja zenye teknolojia hiyo si ajabu tukaona kampuni mbalimbali kwenye orodha miezi inayokuja.

Vyanzo: Gadgets 360, 9to5Mac, GizmoChina

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia.

Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comment

Comments

  1. […] Redmi 9A ni simu janja ambayo hivi karibuni tuu ilitokea kwenye orodha ya rununu ambazo zilifanya vizuri kimauzo mwezi Januari 2021. Je, unafahamu sifa […]

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania