fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

Tanzania TCRA Teknolojia

Usajili wa leseni za maudhui mtandaoni warejea

Usajili wa leseni za maudhui mtandaoni warejea

TCRA ilisitisha kwa muda suala la usajili wa leseni za maudhui mtandaoni tangu Januari 28 ili kuboresha vitu fulani fulani lakini sasa wameanza tena kupokea maombi.

Nchini Tanzania kuwa na “Leseni za maudhui mtandaoni” ni kiutu muhimu sana kwa yeyote yule ambae anafanya shughuli za kuhabarisha watu kwa njia za kidijiti na kufuatia tamko la hivi karibuni kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kuhusu vyombo ya habari vilivyofungiwa na serikali TCRA imeamua kufungua milango na kupokea maombi ya leseni za maudhui mtandaoni.

SOMA PIA  Facebook Wampa Mtoto wa Miaka 12 Dola $10,000 kwa ku'hack Instagram

Usitishwaji huo ambao ungedumu mpaka Juni 30 lakini sasa maombi ya leseni hizo za maudhui mtandaoni  yameanza kupokelewa tangu Aprili 9 2021 na hivyo basi kwa wale ambao watakuwa wamekidhi vigezo kwa mujibu wa kanuni WATARUHUSIWA.

TCRA wanasema kuna kazi ya kitaalamu imefanyika ili kuhakikisha tunasimamia vyombo hivyo ndiyo maana wameondoa zuio.

Kuhusu tozo/ada za leseni za maudhui mtandaoni zenyewe zipo palepale kwa sababu zimewekwa kwa mujibu wa sheria na kanuni kama itakuwa vinginevyo basi itategemea na wizara itakavyoamua.

usajili

Taarifa kuhusu kurejea kwa usajili wa leseni za maudhui mtandaoni.

Haya sasa shime kwa wote ambao tunajishughulisha na masuala ya mtandaoni tupeleke maombi yetu ya kupata leseni lakini kikubwa zaidi tujitathimini kama tunakidhi vigezo kulingana na kanuni zilizowekwa.

Vyanzo: Gazeti la Mwananchi, mitandao mbalimbali

SOMA PIA  Foxconn: Kazi za Wafanyakazi 60,000 zachukuliwa na Roboti! #Teknolojia
Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia.

Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania