Je, wajua kuna muda ambao kosa moja linaweza likajenga kitu cha kitofauti zaidi? Hivyo ndivyo historia ya jina la Google, huduma ya utafutaji maarufu duniani ilivyotengenezwa.
Jina “GOOGLE” liliundwa kwa bahati mbaya mwaka 1997. Hitilafu ya tahajia ilifanywa na waanzilishi ambao walikua na nia ya kuunda neno GOOGOL. Mmoja wa waanzilishi alifanya uchunguzi wa hifadhi data ya usajili wa jina la kikoa cha mtandao (anuani ya .com) ili kuona ikiwa jina lililopendekezwa la “GOOGOL” bado linapatikana kwa usajili na matumizi. Mwanzilishi huyo alifanya makosa kutafuta jina lililoandikwa kama “google.com” ambalo aligundua linapatikana.

Mwanzilishi mwenzake alipenda jina hilo, na ndani ya masaa alichukua hatua ya kusajili jina “google.com” badala ya mpango wao wa kwanza wa kusajili ‘googol.com’.
Ingawa Google halikuwa na maana yeyote kwa wakati huo, neno Googol ndilo lilokuwa na maana kubwa ukilinganisha na huduma waliyokuwa wanakuja nayo. Googol/Googolplex ni neno la kisayansi lenye maana ya utunzaji wa data nyingi, na ndilo jina walilotaka kuipa huduma yao – googol.com.
Kosa la mmoja wao likawakuta wakipenda anuani ya Google.com badala ya googol.com, na kupitia kosa hilo walileta huduma ambayo imefikia kiwango cha kuleta maana ya kipekee. Ni kawaida watu wanapozungumzia suala la utafutaji mtandaoni kwa sasa kutumia neno ‘google’ kama tendo la utafutaji mtandaoni.
No Comment! Be the first one.