Programu ya LeanDroid ya Androidi ni appu moja ya aina yake. Kazi yake ni rahisi – kurefusha maisha ya chaji yako kwenye simu na kukufanya usisumbuke kuwasha na kuzima intaneti.
Unaweza usiamini kusikia hii bila maelezo ila maelezo yake ni marahisi na madogo kama programu yenyewe: Hivi ndivyo LeanDroid inavyofanya kazi:
- Unapofunga skrini, inasubiri dakika kadhaa (utazoamua wewe) alafu inakata intaneti kukurefushia chaji.
- Leandroid itawasha intaneti kila baada ya saa moja (ukiamua) kuruhusu WhatsApp na programu nyingine kutumia intaneti kwa dakika moja kisha itazima intaneti tena.
- Utakapofungua skrini na kuanza kutumia simu, itawasha intaneti kwa raha zako.
Unaamini sasa?
Zaidi ya kukurahisishia kwa namna hii, LeanDroid imetengenezwa kutoingiliana na kazi zako pale unapokuwa unashusha kitu au umeunga simu na simu nyingine au kompyuta (tethering) au kama umejiunga na wayalesi. Pia inaweza kuacha intaneti iwe imewaka wakati unachaji kwa umeme moja-kwa-moja lakini unaweza kuchagua ikate intaneti wakati inachaji kwa kompyuta ili ipate chaji haraka. Chaguzo nyingne ni zile zinazohusu ‘bluetooth’ na unaweza kujipatia uhuru zaidi wa kucheza na chaguzo zingine kama utaamua kuilipia programu hiyo. Unaweza kuona chaguzo hizi zote hapa kwenye hii picha chini.
Ukiangalia kwenye soko la Google Play hauwezi kupata programu nyingine ndogo(248kb kuishusha/ 2.8MB kwenye RAM), rahisi kutumia na bure inayofanya kazi vyema kama LeanDroid kwa sasa. Programu hii inastahili kuwa App ya leo – jipatie hapa au mshirikishe mwenzio – >> Soko la Google Play
No Comment! Be the first one.