fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
Google Intaneti Kompyuta Maujanja Mtandao Teknolojia

Mambo 10 Ya Kushangaza Unayoweza Fanya Ukiwa Google!

Mambo 10 Ya Kushangaza Unayoweza Fanya Ukiwa  Google!

Spread the love

googlr

Google Inc ni moja kati ya kampuni nguli na tajiri sana mtandaoni. Google inapenda sana kucheza na vitu na kubuni mambo mapya kupitia vitu hivyo hasa kiteknolojia. inasemekana pengine ndio kampuni kubwa ya kiteknolojia inayoongoza kwa ubunifu. Licha ya kuwa mafanikio makubwa kampuni hii ina mambo mbalimbali yanayovutia na kufurahisaha.  Leo tutakuonesha baadhi ya mambo ya kufurahisha unavyoweza kuvifanya kupitia Google Search.

Pia logo yake kwenye ukurusa wa Google dot com huwa inabadililika lakini kwa leo hatutaeliweka hili, leo tunakuonesha mambo kumi unayoweza fanya ukiwa Google dot com na kompyuta yako na mengine ata kwenye simu yako.


1. FANYA  PAGE IZUNGUKE KAMA PIPA

Ukiingia katika ukurasa wa google na ukitafuta ‘DO A BARREL ROLL’ page yote itazunguka nyuzi 360

do a barrel roll

2. GOOGLE YA MWAKA 1998

Ukitaka ona jinsi google ilivyokua mwaka 1998 basi tafuta ‘ GOOGLE IN 1998‘ katika ukurasa wa google na utaona muonekano wake kwa mwaka huo jinsi ulivyokuwa

SOMA PIA  SnapChat Waachana Na Kipengele Cha 'Best Friends' Na Kuweka Kingine!

google in 1998

3. ATARI BREAKOUT

Katika ukurasa wa Google tafuta ‘ATARI BREAKOUT‘ kisha yatatokea majibu baada ya hapo bonyeza ‘IMAGES’ litatokea gemu la kubomoa matofari kwa kutumia ki mpira kidogo unaweza ukalicheza gemu hili.

atari

4. ZERG RUSH

Ukiandika neno  ‘ZERG RUSH‘ katika ukurasa wa google , yatakuja majibu vizuri kisa utashangaa vinatokea vi O vingi viingi chini na juu ya kompyuta. vitaanza kula maneno yote yaliyo jitokeza katika hiyo page  kama majibu. ili kuviua vi O hivi inabidi uvibonyeze na Mouse mara  3 kwa mkupuo

zerg rush

5. MVUTONO

Katika Sehemu ya kutafuta vitu katika page ya google andika ‘Google Gravity’  kisha bonyeza ‘I’m Feeling Lucky’  ukisogeza Mouse tuu utaona maneno yaanza kudondoka chini ya skrini yako kuonyesha nguvu za mvutano

gravity

6. JIPANGIE MUDA/DAKIKA

Hii pia inavutia. hivi unajua unaweza kujipangia muda katika ukurasa wa google? ndio unaweza mfano ukiandika ‘SET TIMER FOR 10:30PM‘ inamaanisha hapa ikifika saa nne na nusu usiku kompyuta yako itapiga kelele/mlio kukukumbusha kuwa mda huo umefika, kama alarm/kengere tuu sio?

SOMA PIA  Amazon Inaandaa App (Anytime) Ya Kutuma Na Kupokea Ujumbe/Meseji!

timer

7. TAFUTA KWA SAUTI/KUTAMKA

Sio lazima kila unachokitafuta lazima ukiandike, unaweza pia ukakitafuta kwa kutumia sauti yako. jinsi ya kufanya hvyo, Ingia katika ukurasa wa google alafu tafuta kialama cha kipaza sauti, mara nyingi kinakua mwishoni mwa upande wa kulia katika sehemu unayoandika kitu unachotaka kukitafutakibonyeze kile kisha unaweza sema kitu unachotaka kukitafuta.

voice search

8. VITABU

Kama wewe ni mpenzi sana wa vitabu na unapenda soma basi kuna njia rahisi ya kuvipata. Ingia google sehemu ya kutafuta, Andika ‘BOOKS BY‘ kisha jina la mwandishi au mtunzi, Hapo vitatokea vitabu vyo vya huyo mwandishi/mtunzi

books

9 .SINEMA

Ukiachana na vitabu, je wewe ni mpenzi wa sinema? basi hili litakusaidia pia. ingia ukurasa wa google kisha andika jina la mwigizaji ikifuatiwa na  neno ‘MOVIES‘ hapo zitatikea sinema za huyo msanii kisha utachagua chaguo lako

movies

Mfano wa sinema za Hugh Jackman

10. GOOGLE KAMA KIOO

SOMA PIA  Microsoft inashikilia tovuti zinazotumiwa na wadukuzi wanaoungwa mkono na China

Hii pia ni ya kushangaza, Google inaweza kuwa kama kioo. hii inamaanisha ukiandika maneno yatakua yanaonekana kama yako ndani ya kioo yaani yatakua yamejigeuza, yanaanza kulia yanaenda kushoto. kuona mfumo huu wa kioo bofya hapa

Google Mirror

Hayo ndio mambo 10 ambayo unaweza fanya ukiwa katika tovuti ya www.google.com kwa kumpyuta na mengine ata kwenye simu-janja, mambo haya ni ya aina yake na ya kushangaza kwa sababu  tovuti nyingi hazina ubunifu kama huu. Google bado ipo katika zile kampuni zenye maendeleo sana katika masuala ya teknolojia na inatoa changamoto kwa makampuni mengine kama Apple.

Je makala hii ni ya imekusisimua, tuambie ni kipi umekifurahia zaidi?

Comrade Mokiwa

Mbunifu na mpenda teknolojia.

Muanzilishi wa Teknokona, TechMsaada na Teknokona Group LTD - WWW.TEKNOKONAGROUP.COM

Muda wangu umegawanyika kati ya kazi kibunifu @teknokonagroup na uandishi wa habari za Teknolojia hapa Teknokona Blog.

| mhariri(at)teknokona.co.tz |

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

TeknoKona Teknolojia Tanzania