Wakati teknolojia za vifaa kama vya laptop, tableti na simu zimezidi kukuwa na uwezo wake kiutendaji katika eneo la diski ujazo, RAM na prosesa vikizidi kuwa vikubwa sehemu moja imekuwa bado ni tatizo…nalo ni suala la uwezo wa betri.
Kama unamiliki simu janja basi unafahamu ya kwamba ni lazima uchaji karibia kila siku.
Watafiti kutoka Chuo cha Stanford nchini Marekani wamefanikiwa kutengeneza betri linaloweza kuchachijiwa na kujaa ndani ya dakika moja. Pia teknolojia ya betri hilo ni salama zaidi kuzidi teknolojia ya betri zilizopo sokoni kwa sasa.
Mfano atakama betri hiyo ikitobolewa bado inaweza fanya kazi kwa muda mrefu tuu bila madhara wakati betri zilizopo kwa sasa kama zikiharibiwa wakati zinafanya kazi zinaweza ata kulipuka na kuleta madhara kwa mtumiaji au kifaa husika.
Pia betri hilo litadumu muda mrefu zaidi wakati linatumika zaidi ya teknolojia ya mabetri ya sasa ambayo baada ya kuchaji mara kwa mara yanawahi kuishiwa nguvu ya kuhifadhi chaji muda mrefu zaidi.
Simu za kuweza kujikunja zipo njiani na habari njema ni kuwa betri hili litaweza kukunjwa bila kuathiri utendaji wake. Hakuna Kuvunjika!
Je teknolojia hiyo itaanza kutumika lini? Endelea kutembelea TeknoKona.
SOMA PIA;
Jinsi Ya Kufanya Betri Ya Simu Kuwa Na Maisha Marefu!!
Mambo 6 Yasiyo ya Kweli kuhusu Kuchaji Simu
No Comment! Be the first one.