Mtandao wa Twitter umeleta mabadiliko ambayo kwa wengi yatakuwa ni mabadiliko babkubwa kwelikweli. Kwa muda mrefu imekuwa vigumu kama unataka kuongezea maneno yako pamoja na ujumbe/tweet ya mtu mwingine ndani ya tweet moja.
Kwani sheria ya tarakimu 140 imekuwa inabana sana pale ambapo ujumbe wa mtu mwingine ni mrefu, au maoni yako ni marefu au vyote kwa pamoja. Kwani imekuwa lazima ufuate sheria ya herufi/nafasi 140.
‘Retweet with comment’
Kuanzia leo mtandao huu umerahisisha hili kwani pale unapotaka kuweka maoni yako juu ya tweet ya mwingine tweet hiyo itakuwa ’embeded’ kwenye eneo dogo pamoja na ujumbe wako. Hivyo kwa ufupi kwa sasa utakuwa unapata nafasi zaidi ya mia ya wewe kuandika maoni yako wakati nafasi inayobaki itakuwa na linki ya tweet iliyoi-RT.
Kama mtu akiRT tweet ambayo yenyewe pia tayari imetumwa kwa mfumo huu, yaani yenyewe pia tayari ina ujumbe (RT) mwingine ndani yake basi kitakachotokea ni linki tuu ya kwenda kwenye tweet hizo.
Kwa sasa mabadiliko hayo yashasambaa kwenye app ya Twitter ya simu za iOS na kwenye mtandao wa twitter.com, kwa watumiaji wa app ya Twitter kwenye Android wamesema uwezo huo utakuja hivi karibuni.
Endelea kusoma TeknoKona.Com na jiunge nasi katika mitandao ya kijamii kwa kubofya hapa chini…..
No Comment! Be the first one.