Kwa sasa simu za iPhone 6, Samsung Galaxy S6 Na HTC One M9 ndio simu za juu kabisa zinazoshika bendera katika makampuni hayo husika, na pia zina muamko mkubwa sana katika soko
Wateja wa simu janja hujaribu kuzilinganisha simu hizi kutokana na mapendekezo yao na nini wanategemea katika simu hizo. Japokuwa kuna kitu kimoja cha muhimu sana huwa kinasahaulika kuangaliwa mara nyingi, Je ni simu gani inaweza kutengenezeka kwa haraka kuliko nyingine.
Kwa kuwa vifaa vya kielektroniki huwa vinahitaji matengenezo mara kwa mara kwa sababu nyingi tuu. Kampuni ya kujitegemea ya kimtandao ya iFixit imechukua jukumu la kufanya kazi ya kusaidia watu katika kutengeneza simu zao pale zinapoharibika, Pia kama kampuni limefanya uchunguzi juu ya simu ipi ambao ina uharaka kutengenezeka pale inapopata majanga.
Ipi Rahisi Kutengenezeka iPhone 6, Samsung Galaxy S6 au Htc One M9 pale inapo pata majanga
Tuanze na iPhone 6
iPhone 6 imepata maksi 7 kati ya 10 kwa kuwa na uwezo wa kutengenezeka kiurahisi pale inapopatwa na matatizo mbali mbali
Display (kioo) cha iPhone 6 ndio cha kwanza kutoka pale unapoamua kufungua simu. hii ni njia rahisi ya kutengeneza kioo kama tatizo lako lipo katika kioo. Betri lake ni rahisi kulipata na kulitoa na kulibadilisha lakini ufundi (utaalamu) kidogo unahitajika hapa japokua hakuna ugumu sana,
Pia kebo ya sensa imebadilishwa katika eneo ambalo ilikua inapatikana katika iPhone 5. Hii imerahishisha sana kwa kuwa kwa iPhone 6 nirahisi sana kurekebisha kama kuna tatizo mahali hapo. Mwanzo katika iPhone 5 kebo hiyo ingeweza kuharibika kwa urahisi kama simu isingefunguliwa kwa uangalifu wa hali ya juu
Licha ya kuwa na kiwango cha juu cha kutengenezeka bado Apple hawatoi maujanja haya kwa watu wanaomiliki maduka makubwa ya kurekebisha simu na vifaa vingine vya kielekitroniki.
Kusoma Zaidi: Jinsi Ya Kutenganisha Vifaa Ndani Ya iPhone 6
Sasa Tuingie kwenye Samsung Galaxy S6
Katika Samsung Galaxy S6 iFixit hawakutoa kiwango cha utengenezaji kama walivyofanya katika iPhone. Lakini inaonekana ni rahisi tuu. Kufunfungua kava la betri ni vigumu kidogo lakani inaonekana kuwa kuna kama gundi hivi. Hii inamaanisha kuwa lazima kidogo lipashwa moto (mafundi wanaelewa) ili liweze kuwa rahisi kufunguka.
Pia kuachanisha vifaa kwa umakini kunahitajika ili usiwepo uwezekano wa kuharibu vitu vingine katika simu. Ukiachana na tahadhari tuu za kuchukua kuifungua simu na kutengeneza au kubadilisha vifaa ni rahisi
Kusoma Zaidi: Jinsi Ya Kutenganisha Vifaa Ndani Ya Samsung Galaxy S6
Sasa Ni Zamu Ya Htc One M9
Htc M9 ilipata maksi ya chini kabisa (2 kati ya 10) katika Ifixit hii ikiwa inaonyesha kuwa simu hii ni vigumu sana kuitengeneza pale inapopatwa na tatiozo.
Betri katika kifaa hichi lipo chini ya mazabodi na limewekwa gundi na hili linaleta ugumu katika kutoa ili kuweka lingine. Pia Display (kioo) chake ni vigumu sana kuweka kwa mfano pale kikipasuka, kwa kuwa itakubidi uifungue simu nzima. Zoezi la kubadilisha kioo katika simu hii ni moja kati ya yale magumu.
Htc one M9 pia inaonekana mfumo wake mzima wa ufungwaji ni mgumu hivyo kutoa baadhi ya vifaa katika simu kunaweza hatarishwa maisha ya simu kwa ujumla (Japokua simu nyingi zipo hivyo)
Kusoma Zaidi: Jinsi Ya Kutenganisha Vifaa Ndani Ya Htc One M9
Hitimisho –> Licha ya kuwa tunangojea maksi za Samsung galaxy S6, inaonekana katika simu hizo zingine mbili (iPhone 6 na Htc One M9) iPhone 6 ndio rahisi kutengenezeka.
Kwa kujua yote haya lakini bado kumbuka matatizo (ubovu) katika simu huwa yanatofautiana katika simu na simu
Chanzo ni mtandao wa iFixit.com
Wazo lako ni muhimu, ningependa kusikia kutoka kwako pia tafadhali ungana nasi kupitia kurasa zetu za Facebook ,Twitter, Na Instagram
One Comment