fbpx

Adhabu kutokana na aina ya kosa la mtandao

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Dunia ya leo imekuwa kijiji na kila siku mambo kadha wa kahda yanachapishwa kwenye mitandao mbalimbali lakini kutokana na hilo wenye mamlaka wakatunga sheria ambayo tafsiri yake ikaleta adhabu kutokana na aina ya kosa la mtandao.

Sasa kuna ukweli kwamba si watu wengi ambao wanafahamu makosa ya mtandao kubwa zaidi adhabu ambayo mtu atapewa kulingana na kosa alilotenda baada ya kubainika kuwa umetenda kosa husika. Hizi ndio aina ya makosa ya mtandao pamoja na adhabu zake:

Aina ya kosa la mtandao

Adhabu  ya kosa husika

Udanganyifu unaohusiana na kompyuta Faini isiyopungua Tsh. milioni 20 au mara tatu ya thamani ya fedha inayopatikana kinyume cha sheria/kifungo kisichopungua miaka 7 au vyote kwa pamoja
Wizi wa utambulisho wa mtu binafsi mtandaoni Faini isyopungua Tsh. milioni 5 au mara tatu ya thamani ya faida inayopatikana kinyume cha sheria/kifungo kisichopungua miaka 7 au vyote kwa pamoja
Kutoa taarifa za uongo Faini isiyopungua Tsh. milioni 5 au kifungo kisichopungua miaka 3/vyote kwa pamoja
Picha za ngono (kwa watoto, -18) Faini isiyopuingua Tsh. milioni 50 au mara 3 ya thamani ya faida inayopatikana kinyume cha sheria/kifungo kisichopungua miaka 7 au vyote kwa pamoja
Picha za ngono (kwa wakubwa, 18+)
  • Uchapishaji wa picha za ngono: Faini isiyopungua Tsh. milioni 20 au kifungo kisichopungua miaka 7 /vyote kwa pamoja,
  • Kushiriki kucheza picha za ngono: Faini isiyopungua Tsh. milioni 30/kifungo kisichopungua miaka 10 au vyote kwa pamoja
Unyanyasaji kwa kupitia mtandao

Faini isiyopungua Tsh. milioni 5/kifungo kisichopungua miaka 3 au vyote kwa pamoja

Ujumbe unaotuma bila ridhaa

Faini isiyopungua Tsh. milioni 3 au mara tatu ya thamani ya faida itakayopatikana kinyume cha sheria/kifungo kisichopungua mwaka 1 au vyote kwa pamoja

INAYOHUSIANA  Azam TV yapata leseni ya kuonesha Chaneli za ndani bure

Hiyo ndio tafsiri ya sheria ya mtandao mwaka 2015 kwahiyo kitu kikubwa ni kujiadhari na mkono wa sheria. Jisikie huru kuwashirikisha na wengine ili nao wapate kuhabarika/kuelimika.

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Mhariri Wa TeknoKona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Naomba Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comments are closed.