fbpx

Kenya nayo yafikiria kudhibiti WhatsApp na Skype

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +

ICT CONFERENCE 2019

Sambaza

Serikali ya Kenya inatathmini kudhibiti matumizi ya WhatsApp na Skype katika hatua ambayo inaweza kulazimisha wamiliki wa huduma hizo kutoa habari kwa serikali.

Mamlaka ya Mawasiliano Kenya inatafuta mkandarasi wa kuchunguza na kuamua jinsi huduma hizo zinaweza kudhibitiwa. Mamlaka hiyo inataka kuwa na uwezo wa kudhibiti kama inavyofanya mawasiliano ya simu ya kampuni za mawasiliano ya kawaida.

Wenye mamlaka wamesukumwa kufikiria kuchukua hatua hiyo kutokana na kwamba kampuni hizo kuwa na uwezo wa kupata habari za wateja wao lakini hawana ofisi nchini Kenya.

kudhibiti WhatsApp

Chini ya kanuni za mamlaka ya mawasiliano Kenya wamiliki wa huduma kama WhatsApp na Skype watatakiwa kutimiza ‘Masharti ya usalama na usiri,’ kama inavyohitajika kisheria.

Sheria hizo pia zitajumuishwa kuhusiana na jinsi huduma hizo zitatolewa kuambatana na mahitaji ya mashirika ya usalama kuhusiana na utoaji wa data kama zinavyofanya kampuni kama vile Safaricom inapoagizwa na mahakama.

Chanzo lazima kiwepo.

Uwepo wa WhatsApp umepunguza sana matumizi ya kupiga simu/kutuma ujumbe mfupi wa maandishi; lwa takwimu za mamlaka husika nchini Kenya wastani wa jumbe 96.3 katika kipindi cha Januari-Machi 2018 kutoka jumbe 156.8 kwa wastani katika kipindi cha miezi mitatu mpaka kufikia mwezi Septemba 2017.

kudhibiti WhatsApp

Wakenya wengi wamekuwa wakitumia huduma ya WhatsApp/Skype inayowezesha kutuma jumb na hata kupiga simu kwa njia ya intaneti.

Mamlaka hiyo itatathmini matokeo na mapendekezo ya mshauri na kuamua kuhusiana na masuala ambayo yatatekelezwa katika wajibu wake wa kusimamia mawasiliano.

Facebook Comments

Sambaza

ICT CONFERENCE 2019

INAYOHUSIANA  Ukubwa wa memori ni namba shufwa tu
Share.

About Author

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.

Comments are closed.