fbpx
Android, Huawei, Teknolojia

HongMeng OS: Kufanya kazi kwenye kompyuta, simu, tableti na vifaa vingine

hongmeng-os-kufanya-kazi-kwenye-kompyuta-simu
Sambaza

Programu endeshaji ya HongMeng OS inayotengenezwa na Huawei itatumika kwenye vifaa vingi zaidi ya simu tuu. Hayo yamesemwa na mkurugenzi mkuu wa Huawei katika mahojiano na chombo kimoja cha habari nchini Ufaransa.

Hongmeng OS
Hongmeng OS: Huawei wanategemea kuacha kutegemea toleo la Android kutoka Google ili kuepuka vikwazo vya kibiashara

Mwanzilishi wa Huawei, Bwana Ren Zhengfei amesema kupitia HongMeng OS hawafikirii suala la simu janja pekee, bali wanatengeneza programu endeshaji ambayo itaweza kufanya vizuri pia kwenye kompyuta, tableti na vifaa vingine janja vya kisasa vinavyoitaji programu endeshaji: mfano vifaa vya majumbani, magari n.k.

INAYOHUSIANA  Hadithi App: App Inayokuletea Stori Mbalimbali kwa Wepesi kwenye Simu Yako

Katika mahojiano hayo na gazeti la Le Point Bwana Ren amesisitiza ya kwamba wanaangalia jinsi ya kupunguza utegemezi wao kwa kampuni ya Google.

huawei mwanzilishi
Mwanzilishi wa Huawei: Bwana Ren

Ingawa bado toleo la HongMeng OS halijaanza kupatikana rasmi ila kupitia majaribio wanayoyafanya tayari wamesema wanategemea programu endeshaji hiyo kuwa na utendaji wa kasi zaidi ikilinganishwa na Android na iOS. Ila bado ni mapema mno kuwa na uhakika usiopingika kwenye suala hili.

INAYOHUSIANA  Twitter Lite yaanza kupatikana katika baaadhi ya nchi

Huawei wanategemea programu endeshaji hii itakapokuwa tayari wataanza na soko la China, na kuwekeza katika utengenezaji apps kabla ya kuanza kuitumia kwenye simu zitakazouzwa katika mataifa mengine pia.

Tutaendelea kufuatilia kwa ukaribu maendeleo ya programu endeshaji hii kutoka Huawei. Endelea kutembelea TeknoKona.

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Mhariri Mkuu

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. | mhariri@teknokona.com |