fbpx

Uber Sasa Inaruhusu Kuomba Usafiri Kwa Ajili Ya Mtu Mwingine!

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Tulikua tumeshazoea ile hali ya kwamba tunatumia App ya Uber katika simu zetu na tunaita usafiri ambao unatuhusu moja kwa moja lakini kwa sasa kuna mabadiliko

Kipengele hiki kipya kutoka Uber kinatoa kipaumbele kwa watu ambao wanaelekea uzeeni yaani wale wa miaka 65 na kuendelea.

Inasemekana kuwa asilimia kumi ya watu duniani ni  wazee na jambo hili kampuni ya Uber imeliona na ndio maana imeamua kuja na kipengele  hiki

Lakini kwa upande mwingine sio kwamba toleo hili ni kwa ajili ya wazee tuu bali hata marafiki wa kawaida  na ndugu unaweza ukawaitia Uber

Kitu kinachofanyika ni kwamba wakati unaomba Uber kutatokea na chaguzi likikuuliza kwamba Uber hiyo ije kwako au iende kwa rafiki au ndugu. Ukichagua chaguo la rafiki au ndugu basi itakubidi uchagua namba ya huyo rafiki katika ‘phonebook’ na kisha Uber itamtumia meseji mtu huyo ambayo  ‘link’ ambayo itamuwezesha kufuatilia usafiri huo wa Uber. Taarifa kama nani analipia huduma hiyo na aina ya gari linalokuja vyote vinakua ndani ya meseji hiyo.

INAYOHUSIANA  Huduma za usafiri wa kukodi njia ya anga

Hili ni jambo zuri sana fikiria wewe unaweza ukawa upo Dar lakini ukamuita Uber mtu wa Morogoro na ukalipia kila kitu wewe. hii imekaa poa!

Ningependa kusikia kutoka kwako, hili jipya kutoka Uber unalionaje? niandikie hapo chini sehemu ya comment.

Kumbuka TeknoKona Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.

 

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Mhariri Wa Teknokona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comments are closed.