Katika moja ya pigo ambalo Apple imekumbana nalo ni kuhakiksha vimemeshi vya sinu janja/vifaa vya kidijiti vitumie USB-C (Type-C) na ni kufuatia agizo la Jumuiya ya Umoja wa Ulaya katika kuhakikisha watu wake wanatumia chaji ya aina moja.

Mhandisi Ken Pillonel ameweza kufanya mabadiliko kwenye kitunzo na kifaa cha kujajia earphones za AirPods, kinachofahamika kwa jina la Airpods Case – kuondoa mfumo wa kuchaji wa Lighting, na kuja na mfumo wa Type C.
Mhandisi huyu ameshafanya jambo hilohilo kwenye simu za iPhone X na Samsung Galaxy A51 kwa kupeleka teknolojia ya Type-C kwenye vifaa tajwa sasa inaonekana kuwa anaboresha mikebe ya kubebea/kuchajia AirPods mbali na kuzifanya ziwe zinatumia USB-C lakini pia anaongeza nakshi nakshi ya kuziwezesha ziwe zina wakawaka.

Ingawa Bw. Ken Pillonel anaboresha mikebe ya kwenye AirPods na akiwa ameshafanya kazi kama hiyo kwenye iPhone X na Samsung Galaxy A51 ameifanya michoro yake ya kupeleka Type-C kwenye vifaa mbalimbali vya kidijiti inaweza kutumiwa na mtu yeyote bila kuhitajika kumlipa mwanzilishi wake.
Mabadiliko hayo kwenye AirPods taayari yameshaanza kuonekana kwani watumiaji wake wanaweza kwenda na kubadilisha mikebe hiyo kisha kupewa ambayo ni ya teknolojia ya kisasa zaidi.
Vyanzo: GSMArena, mitandao mbalimbali
No Comment! Be the first one.