fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

Android Apple Teknolojia

Jumuiya ya Ulaya Kulazimisha Chaji za USB-C kwa simu zote

Jumuiya ya Ulaya Kulazimisha Chaji za USB-C kwa simu zote

Spread the love

Ulaya kulazimisha chaji za USB-C kwa makampuni yote ya utengenezaji wa simu. Wanasiasa wa Jumuiya ya Ulaya (EU) wamekuwa wakifanya kampeni kwa zaidi ya muongo mmoja kwa ajili ya kutumia aina moja ya chaja, na utafiti wa Tume ulikadiria kwamba chaja zinazotupwa na zisizotumiwa huzalisha zaidi ya tani 11,000 za taka kwa mwaka.

Katika Jumuiya ya Ulaya, karibu simu milioni 420 na vifaa vingine vya kielektroniki viliuzwa mwaka jana, na mtu wa kawaida anamiliki chaja tatu za simu, ambazo hutumia mbili tu mara kwa mara.

Kwa mwaka 2009, kulikuwa na chaja zaidi ya 30 tofauti, lakini kwa sasa ni aina tatu tu zinazotumika sana ambazo ni: USB-C, Lightning (ya Apple) na USB ndogo-B.

“Kuwa na aina moja ya chaja itakuwa ni ushindi wa busara machoni mwa watumiaji,” Ben Wood, mchambuzi wa CCS Insight alisema.

ulaya kulazimisha chaji za usb-c

Ulaya kulazimisha chaji za usb-c

 

Inaweza kuwa miaka kadhaa kabla ya mapendekezo kuanza kutumika. Tume ya Jumuiya ya Ulaya (EC) inatumai kuwa hilo litatokea ifikapo 2022 ambapo nchi wanachama kwa kawaida huwa na miaka miwili kufanya sheria hizo kuwa sheria ya kitaifa, na watengenezaji watakuwa na miezi 24 ya kubadilisha aina ya chaji zao.

Watengenezaji watalazimika kuunda suluhisho la chaja za simu na vifaa vidogo vya kielektroniki, chini ya sheria mpya iliyopendekezwa na Tume ya Ulaya (EC).Ambapo lengo ni kupunguza taka kwa kuhamasisha watumiaji kutumia tena chaja zilizopo wakati wa kununua kifaa kipya.

“Tulivipa viwanda muda mwingi wa kupata masuluhisho yao, sasa wakati umefika kwa hatua za kisheria kwa aina sawa za chaja. Huu ni ushindi muhimu kwa watumiaji wetu na mazingira kulingana na matamanio yetu ya kutunza mazingira na digitali,” Makamu Rais wa Tume Margrethe Vestager alisema.

Mabadiliko yatafanyika kwenye shimo la kuchajia  la kifaa, wakati mwisho wa kebo inayounganisha kuziba inaweza kuwa USB-C au USB-A.

Apple imeonya kuwa hatua hiyo itadhuru ubunifu. Kampuni hiyo kubwa kiteknolojia na watengenezaji wakuu wa simu janja zinazotumia chaja yao ya kipekee, kwani simu zao za iPhone hutumia chaja aina ya  “Lightning” iliyotengenezwa na Apple.

ulaya kulazimisha chaji za usb-c

Lighting connector, mfumo wa chaja unaotumiwa na Apple kwenye simu zao za iPhone

“Tunabaki na wasiwasi kwamba kanuni kali inayoamuru aina moja tu ya chaja inazuia uvumbuzi badala ya kuhimiza, ambayo nayo itawadhuru watumiaji huko Ulaya na ulimwenguni kote,” kampuni hiyo iliiambia BBC.

Aina mpya za iPad na MacBook hutumia ncha za kuchajia za USB-C, kama vile aina za simu za mwisho kutoka kwa wazalishaji maarufu wa Android kama Samsung na Huawei.

Ni matarajio yetu muda si mrefu Apple itabidi ilete USB-C kwenye simu zake, hili litakuwa jambo jema kwa wateja wao wote ambao tayari wanamiliki vifaa kama iPad au Macbook katika kuwapunguzia mzigo wa chaja nyingi.

Ila pia kwa wao kuwa na USB C kwenye simu zao kutawasaidia ata watumiaji wa simu za Android wenye simu mbili – nyingine ikiwa iPhone, katika kuwapunguzia mzigo wa chaja kwa tofauti.

Vyanzo: Engadget na vyanzo mbalimbali

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania