fbpx
Android, apps, Teknolojia, Telegram

Piga simu katika mfumo wa picha jongefu kwenye Telegram

piga-simu-katika-mfumo-wa-picha-jongefu-kwenye-telegram
Sambaza

Uwezo wa kupiga simu katika mfumo wa picha jongefu sasa umefika kwenye Telegram baada ya watumiaji kuuliza mara nyingi tuu na kwa miaka kadhaa.

Ni miaka minne sasa tangu Teleram waweke uwezo wa mtu kupiga simu kwa njia ya sauti tu na hatimae sasa watu wanaweza wakafurahia kufanya mawasiliano kwa njia ya picha mnato. Vipi nakuchanganya? πŸ˜† πŸ˜† πŸ˜† . Picha jongefu ama mnato ni Kiswahili chaΒ “Video call“.

INAYOHUSIANA  Samsung Hizi Ndio Zinazokubali Teknolojia Ya "Wireless Charging"!

Watu wa kudadavua masuala ya teknolojia tunaamini kwamba Telegram ina vitu vingi vizuri kuzidi WhatsApp ingawa si maarufu sana kama ilivyo kwa mshindani mwenza na pengine wengi wetu tulikuwa tukisubiri kwa hamu kuweza kufahamu kuhusu programu tumishi husika nayo pia iwe na uwezo wa kufanya watu waweze kuonana mubashara.

Ingawa kipengele hicho kimeongezwa kwenye Telegram lakini kinapatikana kwa wanaotumia toleo la jaribio (BETA) na kupakua programu tumishi husika haimaanishi uache kutumia Telegram ama Telegram X la hasha!. Hivyo basi, fahamu kuwa haihitaji kuondoa programu tumishi mama ili mtumiaji aweze kutumia toleo la majaribio linaloruhusu kupiga simu katika mfumo wa picha jongefu.

Picha jongefu
Telegram yawezesha watumiaji wake kupiga picha katika mfumo wa picha mnato ambapo mhusika anaweza akatumia kamera ya mbele/nyuma, kukata sauti au picha, n.k.

Unawaza inapatikana wapi? Jibu ni kwamba Telegram wametengeneza toleo kadhaa ambazo hazipo kwenye Playstore (APKs) hivyo BOFYA HAPA kuweza kupakua programu tumishi husika na uchukue ambayo ni aina namba 7.0.

Hii si ni habari njema kwa wewe ambae unapenda/unatumia Telegram kwenye simu yako? Tupe maoni yako hapo chini.

Chanzo: Android Police

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|