fbpx
Google, Intaneti, Teknolojia

Google kuwezesha mtu kuweka taarifa binafsi mtandaoni

google-kuwezesaha-mtu-kuweka-taarifa-binafsi-mtandaoni

Notice: Trying to access array offset on value of type null in /home/teknoloj/public_html/wp-content/plugins/intelly-related-posts/includes/core.php on line 163
Sambaza

Google ni kampuni ambayo imerahisisha sana watu kuweza kutafuta vitu kwa kutumia teknolojia na pengine isiwe lazima sana kumuuliza mtu kuhusu kitu fulani na badala yake ni kuingia kwenye kivinjari na kutafuta majibu mwenyewwe mtandaoni.

Kwenye jiji la Dar Es Salaam na miji mingine ilyochangamka watu wengi tuu wamepunguza kuulizauliza wapita njia/wenyeji ili mhuhsika aweze kufika sehemu anayokwenda lakini sasa teknolojia imeshika hatamu kwa “Ramani za Google” kuwa ndio mwongozaji wa kutoka eneo moja hadi jingine. Kwanini? Hii ni kwa sababu Google inaruhusu mtu yeyote kuweka anwani ya maeneo mbalimbali ambayo yanawezesha watu kufika sehemu wanayokwenda.

INAYOHUSIANA  App Za Kubadilisha Picha(Wallpaper) ya Simu yako

Inafahamika kuwa kampuni, taasisi, hoteli, n.k wanaweka anwani ya kuwezesha watu kufika mahali walipo lakini tukumbuke kuwa hii ni kwa mgongo wa kitu fulani, si ndio?. Sasa fahamu ya kuwa Google ipo katika hatua ya majaribio kuwezesha watu kuweza kuweka taarifa binafsi mtandaoni.

Yaani mtu ataweza kuweka majina yake, sehemu anapoishi, kazi, namba y simu, tovuti n.k hivi vyote vikimuelezea yeye mwenye na si kampuni/taasisi ama shirika, kwa lugha nyingine ni kama wasifu binafsi wa mhusika.

taarifa binafsi
Kipengele kipya kinachomuwezesha mtu kuweka taarifa binafsi na kupatikana mtandaoni.

Inawezekanaje?

Kipengele hicho kipya kinaitwa “People cards” lakini kwanza kabisa ni lazima utumie akaunti ya barua pepe mathalani “mfano@gmail.com” na baada ya hapo adika kwenye kivinjari “Add me on search” ama “People cards” kwenye Google ambapo mtu ataweza kufungua na kujaza taarifa zake na kuzitunza mtandaoni hivyo kuwezesha kuwa rahisi kumwambia mtu jinsi unavyopatikana/wewe ni nani.

INAYOHUSIANA  Simu rununu Nokia 7.1 imezinduliwa
taarifa binafsi
Polepole naona tunataka kutoka kwenye kumpa mtu kadi ambayo inaonyesha taarifambalimbali zinazokuhusu.

Google wameamua kuanza majaribio ya kipengele hicho kipya nchini India kwanza hivyo basi ni wazi kuwa kwa sasa hakipatikani kwa nchi nyingine. Vipi umepezwa na taarifa hii? Tupe maoni yako.

Vyanzo: The Verge, The Tech Portal

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|