fbpx
Kompyuta, Microsoft, Teknolojia, Windows, Windows 10

Microsoft wazuia Sasisho kwenye baadhi ya kompyuta/laptop: Fahamu sababu

microsoft-wazuia-sasisho-kwenye-baadhi-ya-kompyuta-laptop-fahamu-sababu
Sambaza

Microsoft wazuia sasisho (updates) kwenye baadhi ya kompyuta zinazotumia Windows 10. Sasisho linalozuiwa na Microsoft inasemekana linaweza sababisha matatizo makubwa kwenye kompyuta ambazo zimezuiliwa kuingia.

Kutokana na uamuzi wa Microsoft sasisho la mwezi Mei (May 2019) ambalo tayari limeanza kupatikana halitakubali kwenye kompyuta zote kudownload.

Microsoft wazuia sasisho
Microsoft wazuia sasisho: Jinsi ujumbe kuhusu zuia la kupata sasisho linalojitokeza

Tatizo gani:

  • Kimakosa, sasisho hili linaweza fanya programu endeshaji ya Windows ijichangaye kwenye rekodi za diski au vifaa vya USB vilivyochomekwa kwenye kompyuta husika. Mchanganyo wa rekodi hii inaweza sababisha Windows isiwake/kutambulika au ata data za Diski zingine kuharibika kimakosa.
INAYOHUSIANA  Facebook kuja na Mfumo wa Magemu - kama vile Steam

Masasisho ya Windows 10 yamekuwa mara nyingi yanakuja na matatizo mbalimbali na hili la sasa inaonekana Microsoft wametambua mapema na kuona njia pekee ni kuzuia kompyuta kupokea sasisho hili.

windows 10 microsoft
Windows 10 ni toleo ambalo mabadiliko mengi yanakuwa yanaletwa kupitia masasisho, Microsoft hawatakuja na toleo jingine jipya kwa mabadiliko ya namba tena. Bali mambo mapya yatakuwa yanakuja kwenye njia ya masasisho.

Ukienda sehemu ya kupata masasisha Windows itakupa taarifa kuhusu jambo hili, ila kama kompyuta yako inatumia diski moja tuu (Disk C) basi cha kufanya ni kuhakikisha umechomoa vifaa vingine vyote vya USB wakati unasasisha kompyuta yako.

INAYOHUSIANA  Marufuku matumizi ya Bitcoin nchini Iran

Ushauri muhimu: Kama wewe ni mtumiaji wa kompyuta inayotumia Windows 10 kwa sasa usiwe unapakua masasisho ya Windows 10 mara tuu yanapotoka, ni vizuri kusubiri miezi kadhaa baada kwani matatizo madogo madogo kama haya yanakuwa yameshatatuliwa.

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Mhariri Mkuu

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. | mhariri@teknokona.com |