SoundCloud wamepokea uwekezaji mpya kutoka katika mtandao maarufu wa kijamii, Twitter. Twitter imewekeza dola za kimarekani milioni 70, kutokana na ripoti zinavyosema.
Kampuni hiyo ya kutoka huko Berlin, baada ya kupokea pesa hiyo inasadikiwa kuwa na hadhi ya takribani dola milioni 700 za kimarekani.

Mpaka sasa kwa haraka haraka mtandao wa SoundCloud unatembelewa na watu milioni 175 kwa mwezi. Mtandao huu ndio ule ambao unatoa huduma ya muziki kutoka kwa wasani na ma DJ wachanga bila kuacha wale ambao ni tayari maarufu
Twitter walipoulizwa walikataa kuchangia kitu kuhusiana na jambo hili. Ukiachana na kutofanya vizuri kwa kampuni ya SoundCloud bado Twitter lengo lao halikufa. Kumbuka kati ya mwaka 2012 na 2013 kampuni ya soundcloud ilipata hasara ya kiasi cha dola milioni 70 za kimarekani
Mwanzoni mwaka huu kampuni iliamua kubadilisha mfumo wake mzima na pia ukafanya maboresho kwa kuanzisha huduma ya muziki wa ku ‘Stream’ kwa malipo kwa kipindi Fulani (Mwisho wa mwezi, mwaka n.k)

Licha ya SoundCloud kufanyaga vibaya lakini bado wataalamu wa mambo ya teknolojia wanatabiri kuwa bado mtandao huo utazidi kupeta tuu.