fbpx
apps, Facebook, instagram, Snapchat, whatsapp

Watumiaji wa Facebook Stories wafikia milioni 500: Sawa na Instagram na WhatsApp Stories

watumiaji-wa-facebook-stories-milioni-500
Sambaza

Watumiaji wa Facebook Stories wafikia milioni 500 na zaidi. Hii ni idadi inayofikia apps zingine kama vile WhatsApp na Instagram, kwenye eneo la Stories apps hizi pia zinawatumiaji zaidi ya milioni 500.

Kwenye apps za mitandao ya kijamii ni app ya Snapchat ndio ilikuja kwa mara ya kwanza na ubunifu wa huduma ya stories. Baada ya juhudi za mara kadhaa za Facebook kuinunua app ya Snapchat bila mafanikio wakaona jambo pekee lililobakia ni kuipa baadhi ya ubunifu spesheli uliokuwa kwenye app ya Snapchat. Na hapa ndio wakaiba ubunifu wa stories na kuuingiza kwenye app zingine.

INAYOHUSIANA  WhatsApp: Mambo Ambayo Huenda Huyafahamu

Watumiaji wa Instagram Stories kwa siku walivuka kiwango cha watumiaji milioni 500 kwa siku miezi kadhaa nyuma, watumiaji wa WhatsApp Status pia walifikia idadi hiyo pia wiki kadhaa zilizopita.

Watumiaji wa Facebook Stories
Watumiaji wa eneo la stories kwa apps za Facebook, WhatsApp, Snapchat na Instagram

Facebook Stories zinaweza kutazamwa kupitia huduma ya Facebook na Facebook Messenger.

Uamuzi wa Facebook kuiba ubunifu wa huduma ya stories kwenye app zake umeonaka kuleta hasara kubwa kwa ukuaji wa app ya Snapchat. Tokea huduma ya stories ianze kupatikana kwenye familia ya apps za Facebook imesababisha ukuaji wa Snapchat stories kuporomoka. Kwa sasa watumiaji wa Instagram Stories ni takribani milioni 190 kwa siku – chini ya nusu ya wastani kwa apps za familia ya Facebook.

INAYOHUSIANA  Netflix ya Magemu? Microsoft waja na huduma ya malipo ya mwezi, magemu 100+
FB Stories

Facebook wapo njiani kuwapa watangazaji matangazo mfumo rasmi wa kutangazo moja kwa moja kupitia eneo la Stories linazopatikana kwenye apps za Instagram na Facebook.

Je unatumia app gani zaidi kwenye kuweka picha/video kwenye eneo la stories?

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Mhariri Mkuu

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. | mhariri@teknokona.com |