fbpx

Tabiti: Ifahamu Samsung Galaxy View 2

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Samsung ambao wana bidhaa lukuki sokoni kutoka familia mbalimbali ambazo zinapata wateja lakini bila kusahau ushindani sasa kampuni hiyo imeamua kutoa kimya kimya tabiti yao ambapo sio mara kwa mara zinatoka.

Soko la tabiti sio maarufu sana kulinganisha na simu janja pengine hii inasababishwa na kile ambacho wateja wanavutiwa nacho katika kipindi hicho na kwa hali inavyoonekana rununu/simu janja ambazo zina umbo dogo ndio zinazovutia zaidi kwenye soko la ushindani ukilinganisha na tabiti. Haimaanishi kuwa soko la tabiti linapotea, la hasha! Kwani Samsung wametoa Samsung Galaxy View 2.

INAYOHUSIANA  Simu ya Pixel 3A na 3A XL - Google waja na Simu ya Pixels kwa bei 'rafiki'

Je, ina sifa gani?

Kama tunavyofahamu tabiti huwa hazina mbwembe nyingi na hivi katika pita pita zangu huku na kule nikapata kujua sifa za tabiti husika; ni sifa rasmi ingawa bidhaa husika tayari imeingia sokoni tangu Aprili 26. Undani wa tabiti husika ni kama ifuatavyo:-

Muonekano/Kiori mama: Kwa muonekano kioo chake kina urefu wa inchi 17.3 (ung’avu wa muonekano wa kitu ni ubora wa 1080px) hivyo basi kwa wale tunaopenda tabiti pana hapa tutakuwa tumefurahi. Vipuri mama (8 ndani ya 1) Samsung wameamua kutumia Exynos 7884 SoC yenye kasi ya 1.6 GHz.

INAYOHUSIANA  Kuwa Makini App Za Bure Zinaweza Kuiba Data Zako!

Kamera: Kamera zote (nyuma/mbele) zina MP 5.

Samsung Galaxy View 2

Samsung Galaxy View 2

RAM/Memori ya ndani: Tabiti hiyo inakuja na RAM GB 3, diski uhifadhi GB 64 lakini pia uwezo wa kuweka memori ya ziada mpaka GB 400.

Betri/Mengineyo:Betri yake ina 12000mAh, inatumia USB Type C, Samsung Galaxy View 2 inatumia Android Oreo, kuna spika tatu pamoja na sehemu ya kuchomekea spika za masikioni, rangi ni kahawia iliyopauka, ina kutumika katika mfumo wa runinga na inakubali mtandao wa 4G LTE.

INAYOHUSIANA  Baada ya iPhone 6 Plus, Apple kuja na iPad Pro

Samsung wameamua kuzindua bihaa hiyo kimya kiya ambapo inauzwa kwa $740|zaidi ya Tsh. 1,739,000 lakini kupitia AT & T unaweza ukalipia kidogo kidogo ($37/mwezi ndani ya miezi 20).

Vyanzo: Neowin, GSMArena

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.