Chrome 74: Jinsi ya kuweka muonekano wa giza kwenye simu/kompyuta

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Kutumia muonekano wa giza kwenye programu mbalimbali sio itu cha ajabu kwa watu ambao wanapenda kupekua vitu na kutaka kufahamu vitu mbalimbali. Kitu hicho kipya kimevutia makampuni mengi kutokana na vitu vinavyoonekana iwapo programu husika ikiwa katika mfumo huo.

Google Chrome ni moja ya kivinjari/programu tumishi ambayo ilikuwa bado haijaongeza kipengele hicho mpaka toleo la Chrome 74 kote kwenye simu na hata kompyuta ingawa wamua kutofanya kipatikane kiurahisi; ni lazima uongeze vitu fulani fulani uweze kupata mpangilio husika.

INAYOHUSIANA  Teknolojia ya magari ya umeme yaingia Serengeti

Kwenye simu janja (Android)

Kwa anayetumia simu janja ya Android na anatumia Chrome kama kivinjari itambidi kufungua kivinjari husika na kuchapisha “chrome://flags/#enable-android-night-mode” kwenye shemu ya kuandika tovuti kisha bofya “Go/Ok“. Ukurasa mpya utafunguka na hapo utakwenda moja wa moja kwenye kipengele cha “Dark Mode” na kukiruhusu.

Iwapo hautapendezwa na muonekano wa giza kwenye kivinjari cha Chrome kwenye Android unaweza ukarudisha kama ilivyokuwa hapo awali kwa kuingia kwenye mpangilio (settings ndani ya Chrome) kisha nenda kwenye kipengele cha “Dark Mode” halafu chagua “Default” au “Disabled“.

Chrome 74

Jinsi ya kuruhusu muonekano wa giza kwenye kivinjari cha Chrome 74 kwa simu za Android.

Kwenye kompyuta

Kipengele hiki cha muonekano wa giza pia kimewekwa kwenye kivinjari husika kwa wale waokitumia kwa njia ya kompyuta kupitia Windows 10, Mac na hata Linux  lakini inabidi uongeze kitu kidogo ili kuweza kuruhusu kitu hicho. Inakupakupasa ufanye yafuatayo:-

INAYOHUSIANA  Samsung njiani kufungua viwanda zaidi nchini Marekani

bofya kitufecha kulia kwenye kipanya pale palipoandikwa “Google Chrome Shortcut” kisha ongeza “–force-dark-mode” (bila ya kuweka alama ya funga/fungua semi) kuweza kupata muonekano wa giza kwenye Chrome 74 ya kompyuta.

Chrome 74

Muonekano wa giza kwenye Google Chrome (kompyuta).

Hivyo ndivyo walivyoamua kufanya kivinjari cha Chrome katika muonekano wa giza (kwenye simu janja/kompyuta) kiweze kupatikana. Sasa kazi ni kwako wewe ambae utahitaji kubadilisha kwa kufuata maelekezo hatua kwa hatua.

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.