Watu wengi wakifikiria kutengeneza programu tumishi basi wanafikiria watu wanaotumia simu za Android au wakati mwingine toleo la iOS/Android zote zikawa zinapatikana kwa wakti mmoja lakini hii haimaanishi soko hilo la programu tumishi (Google Playstore/App Store) halipewi jicho la karibu na wahusika.
Kabla ya programu tumishi kuweza kupatikana kwa watu kuweza kuishusha kwenye Android/iOS ni lazima ipitiwe na wahusika kisha wakiipitisha au kuikataa aliyeitengeneza anapewa taarifa kuhusiana na ombi lake. Wakati mwingine hata kama programu tumishi inapatikana kwenye soko husika inaweza kuondolewa wakati wowote kutokana na sababu mbalimbali.
Programu tumishi zipatazo arobaini na sita (46) zilizotengenezwa na kampuni moja nchini Uchina zimeondolewa kwenye Google Playstore mara baada ya kubainika kutumia mbinu za uongo kwenye matangazo ambapo iliyokuwa ikionyesha mtu amebofya tangazo fulani lakini kube si kweli ili kuweza kujipatia kipato kwani matangazo ndani ya progamu tumishi ni chanzo cha mapato kwa wengine.
Programu tumishi 46 zote zilikuwa zimepandishwa na watu tofauti tofauti lakini kumbe nyuma ya pazia zimetengenzwa na DO Global (kampuni) na tayari zilikuwa zimeshapakuliwa na mamilioni ya watu.
Tujiadhari sisi tunaotengeneza programu tumishi kwani usifikiri kwamba iwapo imekubaliwa (kuwekwa sokoni) basi unaweza ukaanza kufanya mambo yasiyofaa, kuna macho mengi na ikibainika tu na wakajiridhisha kuwa kuna ndivyo sivyo inaendelea programu husika inaondolewa.
Timu ya uandishi wa Kona ya Teknolojia ingefurahi kupata sapoti yako ili iendelee kukuletea habari na maujanja mbalimbali.
Wezesha bando kwa kutuma kiasi chochote kupitia Selcom, kwenye simu yako bofya *150*50*1# kwenye namba ya malipo weka 60751369 jina litakuja TEKNOKONA.
Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia.
Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|