Youtube ni mtandao ambao kila leo unazidi kuwa maarufu na kuzidi kuwa na mashabiki wengi. Tumeona watu mbalimbali wakiwa na chaneli zao binafsi huku wakiwa na uwezo wa kuweka video kwenye Youtube na watu kuangalia video kupitia wao. Je, unajua waliwezaje kufanikisha hilo?
Mtu yeyote anaweza kuwa na Youtube chaneli yake binafsi hivyo kuweza kuweka video mbalimbali na watu kuweza kuona hivyo kujulikana na hata kulipwa kutokana na idadi ya watu wanaotazama video zako (views). Jambo la msingi na muhimu kuzingatia ni kuwa na barua pepe na kama hauna basi ni muhimu kuwa nayo.
Hatua za kufuata wakati wa kutengeneza akaunti kwenye Youtube chaneli.
- Tembelea tovuti ya Youtube. Upande wa kulia juu una sehemu mbili; kama hauna barua pepe au kama tayari una barua pepe ya Gmail unabonyeza “Sign in”.
2. Baada ya kusign in bonyeza “My channel” kisha bonyeza “Use a business or other name“. Hapa utaweza kutengeza akaunti yako ya kibiashara kwenye Youtube. 3. Chagua jina lako la kibiashara. Hapa ndio sehemu muhimu sana kwani lazima uchague jina rahisi ambalo litakuwa ni rahisi kukumbuka. Ni muhimu sana jina lako la kibiashara lisiwe refu.
Kumbuka kuweka video ambazo hazitakuleta matatizo ya kuwa na hakimiliki ili kuepuka matatizo mbalimbali ya mitandaoni na kuanza kuingiza kipato bila ya wasiwasi cha msingi tu watu kutazama video unazoziweka.
Vyanzo: Hootsuite, Lifewire