Google na kampuni nguli ya ubunifu wa mavazi, Levi’s, kwa kushirikiana pamoja wameleta jaketi janja linalofahamika kwa jina la Jacquard.

Jaketi hili lina teknolojia ndogo ndogo za elektroniki ndani ya kitambaa chake na kifaa kingine cha nje na hivyo kumuwezesha mvaaji kuweza kuchukua hatua mbalimbali zinazohusisha simu yake moja kwa moja kwa kushika sehemu flani za koti hilo.
Teknolojia gani hasa inaunganisha koti na simu yako?
Koti linakuja na teknolojia ya Bluetooth na hivyo mvaaji inabidi aunganishe mawasiliano ya kati ya simu na koti hili. Mfano kama mtumiaji anataka kuanzisha mziko kucheza au kuusimamisha (pause) basi anaweza kugusa mara mbili eneo flani la koti hili na hicho kitafanyika moja kwa moja.

Vingine utakavyoweza kufanya kupitia koti la Jacquard;
- Kupokea simu
- Mambo yote muhimu yanayohusisha apps za kusikiliza muziki
- Kupata maelekezo ya mahali (directions) etc
Hizi ni teknolojia ambazo kawaida ungeziona kwenye filamu ila Google wakishirikiana na Levi’s wanaonesha ni jambo linalowezekana na tulitegemee sana tuu katika miaka inayokuja.
Kutakuwa na kataa chochote kanakowaka?
Hapana, kampuni ya Levi’s imesema wateja wa nguo zao ni watu ambao wasingependa kuvaa nguo ya namna hiyo – yenye vijitaa taa. Na hivyo teknolojia iliyotumika ndio maana imekuwa ndogo sana kiasi cha kutosha kushonewa ndani ya mavazi haya – kwa kuanzia ni makoti. Eneo pekee litakalokuwa linauwezo wa kubadilika rangi kulingana na kinachoendelea kwenye simu yako ni kimkanda kidogo ambacho kinauwezo wa kuvishwa na kuondolewa kwenye nguo.
Kimkanda hichi peke yake akiwezi kufanya kazi, kinategemea teknolojia iliyokwenye nguo.
Utaweza kuliosha?
Kuna kidude kidogo kitakachokuja pia na nguo hiyo kinachochomekwa kitakuwa na uwezo wa kuondolewa kutoka kwenye nguo yako. Pale utakapoondoa kipande kidogo sehemu zingine zote za nguo utaweza kufua bila tatizo.
Bei?
Makoti ya Jacquard yataanza kupatikana kipindi flani mwaka huu (Mwezi wa tisa – kumi) na bei ya takribani laki 7 (USD 350).