fbpx
Infinix, simu, Teknolojia

Fahamu Teknolojia Ya Infinix NOTE 7!

fahamu-teknolojia-ya-infinix-note-7
Sambaza

Kupitia kurasa zao pendwa za mitandao yao ya kijamii kampuni ya simu ya Infinix imezindua rasmi sifa za simu mpya aina ya Infinix NOTE 7 au unaweza iita BIGIMAKINI.

Infinix NOTE 7 ni simu yenye sifa lukuki zenye kuvutia kuanzia umbo lake kubwa lenye upana wa kioo cha nchi 6.95 na megapixel 48 kamera pamoja na kasi ya processor aina ya MediaTek Helio G7

Muonekano Wa NOTE 7 Kutoka Infinix
Muonekano Wa NOTE 7 Kutoka Infinix

Processor ya G70 inakasi kubwa yenye kuwezesha matumizi mbali mbali ya kiofisi na yasiyoyakiofisi kama vile games zinazoitaji speed kubwa bila kuchoka na miongoni mwa sifa nyengine za NOTE 7 ni uwezo wa kukaa na chaji kwa muda mrefu pasipo uhitaji wa kuichaji kwa muda mwingi kutokana na uwezo mkubwa wa battery yenye mAh 5000 na teknolojia ya fast charge. Sifa yingine zenye kuifanya Infinix NOTE 7 kuwa simu yako bora kwa mwaka huu wa 2020 ni ukubwa wa memori ya diski uhifadhi GB 128  na RAM ya GB 6

INAYOHUSIANA  Xiaomi yafungua zaidi ya maduka 500 kwa wakati mmoja
Betri La NOTE 7 Hudumu Zaidi
Betri La NOTE 7 Hudumu Zaidi Kwa Kukaa Na Chaji Muda Mrefu 

Kwa mwaka huu wa 2020 NOTE 7 ndio simu kubwa zaidi kutolewa na kampuni hii ya Infinix lakini kutoka na ugonjwa ambao unaikumba dunia nzima kwa ujumla Infinix imelegeza bei kwa wateja wake na simu hii itapatikana madukani kwao Infinix Smart Hub Mlimani City na Smart Hub Kariakoo kwa bei isiyozidi 480,000 za kitanzania.

NOTE 7 iko vizuri pia katika maswala ya 'Games'
NOTE 7 iko vizuri pia katika maswala ya ‘Games’

Vile vile Infinix inakupa nafasi ya kujishindia Infinix NOTE 7 nyingine mpya kwa mteja yoyote wa Infinix NOTE 7 atakayepiga picha box la simu baada ya kununua na kupost kwenye mtandao  wa kijamii na kuambatanisha na #tag ya #BIGIMAKINI, na zawadi nyengine kama vile magic cup, Notebooks, Speaker hutolewa papo hapo.

INAYOHUSIANA  'IP Address' Ni Nini? Fahamu kuhusu teknolojia hii muhimu

Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika eneo la maoni, hii umeipokeaje? kumbuka kutembelea mtandao wako pendwa wa TeknoKona kumbuka daima tupo nawe katika tekolojia!.

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Hashdough

Mhariri Wa TeknoKona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Naomba Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com