fbpx

Serikali ya Uchina na magari yanayotumia umeme

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Uchina kama taifa kubwa linaongoza kwa kuwa na magari yanayotumia nishati ya umeme kama mbadala wa kukabiliana na uchafuzi wa mazingira na makampuni yanayotengeneza vyombo hivyo vya yamekuwa yakipata soko kwa wingi tuu.

Taifa kubwa lenye uchumi imara lakini pia likwa moja ya nchi yenye watu wengi duniani inafahamika vyema kwa kufuatilia watu wanaoishi nchini humo kwa kutumia mbinu mbalimbali ambapo serikali husika ina malengo yake.

Kwa muda mrefu tuu serikali ya Uchina imekuwa ikitaka kupata taarifa za watu wanaomiliki magari yanayotumia nishati ya umeme na kuanzia mwaka 2017 ikawa ni lazima kwa makampuni hayo kutoa taarifa hizo ambazo zinajumuisha mahali mtu alipo kwa wakati huo, sehemu anayoishi, n.k.

Uchina ina makampuni zaidi ya mia mbili (200) ambayo yanatengeneza magari yanayotumia umeme na mengi kati hayo yamekiri kutoa taarifa za wateja wao kwa serikali husika kwa madai kwamba ni kwa manufaa ya wananchi.

magari yanayotumia umeme

Nchi zinazoongoza kwa kuuza magari yanayotumia nishati ya umeme-Ripoti ya mwaka 2017.

Makampuni hayo yanasema wateja wao wanajua jinsi gani taarifa zao zinavyotumika.

Wenye mamlaka wanasema hatua hiyo inasaidia kuondoa udanganyifu kwa programu inayohamanisha watu kutumia magari ya umeme huku wakipata punguzo kubwa kwenye makato mbalimbali.

Vyanzo: The Verge, Extreme Tech

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  Mfumo wa kuhakiki mtu kwa mishipa ya mkono wadanganyika
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.