iPhone nyingi watu wanazifurahia sana kwani zina karibia kila kitu ambacho kinahitajika kwa simu janja, lakini wengi wanasema tatizo ni betri katika simu hizo. Ni kweli chaja ni muhimu sana katika simu na simu janja nzuri ni ile amabayo chaja haaishi haraka.
Kumbuka bado kampuni imeweka njia nyingi za kuhakikisha kwamba zinasaidia kulisoma betri na saa zingine mtumiaji anaweza mpaka akaiamuru iPhone yake kula chaja kwa uchache sana kuliko kawaida, kipengele hichi kinajulikana kama ‘Lower Power Mode’

Lakini ukifikira vizuri licha ya kipengele hichi kuwepo bado mambo ni mengi na kwa kiasi fulani unaweza sema kipengele kina mchango mdogo, vile vile hawakuishia hapo kuna baadhi ya hataua ambazo wamezipiga ili kukabiliana na hili.
Lakini vyanzo mbali mbali vinasema kuwa Apple wana simu zenye maumbo membamba hali ya kwamba inafanya betri la simu (ndani) liwe jembamba hali ya kwamba pia hata uwezo wake wa kukaa na chaja utakua mdogo tuu.
Apple wametoa njia ambazo kwa namna moja au nyingine zitakusaidia ili kuhakikisha betri la simu yako linakaa asilimia 100 kwa kipindi cha muda mrefu.
Kumbuka Apple wanadai kuwa maisha ya betri (betri life) ambayo yanapimwa kwa asilimia ni namna tosha au njia tosha ya kujua maisha ya betri hiyo mpaka pale utapokwenda kubadilisha betri ingine.

Apple wanadai kuwa joto pia lina athari katika betri, na betri za simu zao huwa zinafanya kazi vizuri zaidi zikiwa katika degri 16 mpaka degree 22 za sentigredi (celsius) na pia inabidi mara nyingi kukwepa sehemu ambazo zina sentigredi 35+
Njia Zingine Za Kuhakikisha Ufanisi Wa Betri Ni Hizi!
- ‘Lower Power Mode’
Hii ni kama nilivyoigusia kidogo pale juu
- Usipendelee kuacha baadhi ya App kula data pasipo wewe kuzitumia (Backgroud App refresh) ukiingia katika settings, nenda katika general na kisha ingia katika Background App Refresh
Kuna njia nyingine nyingi ambazo unaweza kuzisoma hapa
ILI KUJUA KAMA NJIA HIZO ZINAFANYA KAZI IPASAVYO
Sasa umeshaweza kuhakikisha kwamba unatunza vipi betri lako, sasa utajuaje kama njia hizo zinafanya kazi kama inavyopaswa? ni wazi ni lazima uende ukachungulie kama asilimia za maish aya betri zinashuka sio?
Ingia katika settings na kisha na tafuta neno Battery wakati unashuka chini….ingia humo na kisha Battery Health ambapo hapo unaweza onyeshwa maisha ya betri lako yalipofikia.

Kingine cha muhimu ni kwamba ukiwa unabadilisha betri la simu inabidi kuhakikisha kuwa unapata vifaa ambavyo ni bora na vinaaminika na kuepuka mabetri ambayo ni ‘used’.
No Comment! Be the first one.