Ufaransa imesema kwamba inampango wa kuhakisha kunakuwa na keyboard ya aina moja inayotumiwa nchini humo ambayo haitafanya uandikaji wa Kifaransa fasaha kuwa mgumu.
Tofauti na nchi kama Marekani na Uingereza ambako keyboard inayotumiwa ni ile ya QWERTY Ufaransa wanatumia keyboard aina ya AZERTY lakini hizi hazijawekwa katika viwango vya pamoja jambo ambalo limesababisha zitengenezwe keyboard za aina hii zenye tofauti nyingi.
Kifaransa kinatumia elufi spesheli (special characters) kwa wingi na kuwa na keyboard spesheli ni muhimu sana kwa ajiri ya kurahisisha uandikaji na kuleta maana. Keyboard zinapotofautiana watumiaji wengine hushindwa kuziona herufi hizi maalumu na hushia kuandika Kifaransa kigumu kitu ambacho Ufaransa inataka kupunguza.
Ingawa idadi ya watu wanaoongea Lugha hii imezidi kuongezeka duniani lakini pia makosa madogo madogo ya kisarufi na ki msamiati yamekuwa yanaongezeka zaidi. Mijadala mingi juu ya kuongezeka kwa makosa katika kifaransa inaoneshea utofauti wa keyboard kwa upande mmoja lakini pia kwa upande mwingine inaonekana pia matumizi ya mitandao ya kuchati inaweza kuchangia watu kuongea Kifaransa kisichofasaha.
Viwango hivi vipya vitakapo kuwa vimewekwa vitatumiwa na watengenezaji wa keyboards kwa hiyari, lakini itakuwa ni lazima kwa maeneo ya uma kuwa na kompyuta zenye keyboard zinazokizi viwango hivi.
AFNOR ndiyo kampuni iliyopewa kazi ya kutengeneza viwango vya keyboard na hivyo itaweka viwango vya utengenezaji wa keyboards, na tayari kampuni hii imeshakwisha sema kwamba yeyote anayetaka kushiriki anaweza kushirik katika utengenezaji huo.
No Comment! Be the first one.