Kumbuka tovuti (website) nyingi zina mionekano miwili yaani ule wa kwenye simu janja na ule wa kwenye kompyuta.
Kingine cha kufahamu katika hili– website — ni kwamba unaweza ukawa na uwezo wa kulazimisha muonekano wa tovuti wa kwenye kompyuta uonekane katika simu janja.
Ni wazi kwamba kuna vitu vingi ambavyo unaweza kuvipata katika kompyuta na katika simu janja ukavipata vile vile lakini kuna vingine vinaweza kuwa ni mtihani kidogo.
iPHONE
Ukishakuwa umeingia katika tovuti yeyote kupitia katika simu ya iPhone nenda katika eneo lenye herufi Aa (Hakikisha unatumia iOS 13 na kuendelea).
Ukishaingia hapo utakua na uwezo kuchagua machaguo mengi moja wapo likiwepo ni kuchagua muonekano wa kompyuta (Request Desktop Website).
Hiyo ni kama unatumia kivinjara cha Apple (Safari) lakini kama unatumia kivinjari kingine kama vile Google Chrome utaweza kuingia katika vile vidoti vitatu na kisha chagua “Request Desktop Website’’
ANDROID
Hapa sasa kwa kuwa simu zote za Android zina kivinjari cha chrome, tutumie hicho hicho kuelezea swala hili.
Kwa kutumia kivinjari hiko ingia katika tovuti na kisha nenda kwenye vidoti vitatu na kisha chagua “Desktop Site’ ili kuweza kufanikisha hili.
Ni wazi kwamba kuna vivinjari vingi sana ambavyo vinaweza kutumika katika Android lakini vingi vyao unaweza tumia njia hii hii –ya chrome—katika kuhakikisha kuwa unaliwezesha hili.
JINSI YA KURUDI KATIKA MUONEKANO WA SIMU
Kwa kutumia njia zile zile ulizotumia kuingia katika muonekano wa kompyuta ndio njia hizo hizo unaweza kuzitumia katika kuhakikisha kuwa unarudi katika muonekano wa simu.
Njia hii ni moja kwa mifumo yote yaani Android na iPhone maana unakua unafanya njia zile zile ila unakua kama unaenda kinyume na ulivyofanya mwanzo.
NIngependa kusikia kutoka kwako, je unadhani hii inasaidia sana katika kuhakikisha mtu anapata muonekano anaoutaka katika kifaa chake? Au hii haina maana sana?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.