fbpx
Kompyuta, Mac, Maujanja, Teknolojia

Kompyuta: Ubora uleule lakini faili ni dogo

ubora-uleule-lakini-faili-ni-dogo
Sambaza

Mara nyingi inakuwa ni ngumu kudogo kwa wengi wetu kuweza kufanikisha kupunguza ukubwa wa faili lakini ukiwa na lengo kwamba ubora wake usipungue.

Programu mbalimbali kupitia kompyuta zinaweza kufanya mengi ambayo mengine pengine uliwahi kufikiria kuwa haiwezekani kufanikisha na kama sio mtu wa kutaka kujua mengi basi unabaki na fikra isiyokuwa ya kweli.

Kompyuta za MacBook ni moja ya bidhaa za Apple ambazo si rahisi kujua mengi kirahisi kama ilivyo kwenye vifaa vingine vinavyotumia Windows. Naamini ungependa kujua namna gani unaweza kupunguza ukubwa wa kitu (hasa picha jongefu) bila kupoteza ubora wa picha.

INAYOHUSIANA  Misheni ya kwenda katika mfumo wa Nyota nyingine yazinduliwa

Kwa kutumia VLC Player

Ptogramu hii ni maarufu sana kwa wengi lakini pia kuna mengi ambayo yanaweza kufanyika kwa kutumia VLC Player ila hivyo hatujui. Sasa pale unapotaka kupunguza ukubwa video utabofya kwenye Media>>Convert/Save>>Add ili kuweka hiyo video ambayo unataka ipungue ukubwa.

Ubora uleule
Ukishafanikisha kuweka video ambayo umedhamiria kuibadilisha bonyeza neno “Convert/Save”.

Kiini cha zozi zima ni pale ambapo sasa imefikia hatua ya kuchagua ubora ambao unataka vudeo hiyo uwe nayo mara baada ya kuipunguza. Inashauriwa uchague “Video for MPEG4 1080p TV/device” (ukubwa wake utakuwa ukubwa usiozidi MB 70-MB 80) au “MPEG4 720p TV/device” (ukubwa wake utakuwa kati ya MB 40-MB 50).

Ubora uleule
Ukishachagua ubora utakaopenda sasa itakubidi uamue sehemu ya kuhifadhi faili husika (Destination file) kisha ubofye “Start”.

Zipo programu nyingi lakini kimsingi ukitumia VLC Player itafanya kazi ya kupunguza faili (picha jongefu) kwa urahisi zadi na kuwa na ubora uleule. Kumbuka kuwa mvumilivu wa dakika kadhaa kuacha zoezi likamilike.

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|