Kampuni ya SEGA ni moja kati ya makampuni makubwa sana na ya muda mrefu kabisa katika tasnia ya magemu na kwa sasa inaitolea macho kampuni ya Rovio ambayo ndio watengenezaji wa gemu ya Angry Birds.
Kwa upande mwingine nayo Gemu ya Angry Birds ni moja kati ya magemu ambayo yamejipatia umaarufu mkubwa sana na kwa upande limetengeneza pesa nyingi sana.
Dili hili linasemekana kwamba linafikia mpka dola za kimarekani bilioni moja na hii ni kwa kulinunua kampuni hilo la Rovio.
Maongezi haya ya kampuni hizo mbili yamechukua muda kidogo mpaka kuja kufikia hapa, mwanzoni kabisa kampuni ya Rovio iliweka wazi kwamba kutakua na mabadiliko katika kampuni hiyo na inaweza ikatokea ikauzwa.
Kampuni ya SEGA ni maarufu kwa magemu yake ya Sonic the Hedgehog ambayo kwa muda mrefu yamekua yanafanya vizuri sana mpaka kupelekea kuletwa filamu zinazotumia jina hilo.
Kampuni ya Rovio sio mara yake ya kwanza kutaka kununuliwa na kampuni nyingine lakini mara kwa mara jambo hili halikufanikiwa.
Angry Birds ilianza na kuwa maarufu sana mwaka 2009 kupitia kampuni hiyo ya nchini Finland na ndio gemu ya kwanza kabisa kushushwa (download) mara bilioni moja.
Kuna matoleo mengi sana ya mchezo huu, Angry Birds na mpaka sasa kuna matoleo mawili ya filamu ambazo zinahusiana kabisa na mchezo huu.
Mpaka mwaka jana kampuni ya Rovio imejigamba na kusema kwamba michezo yake mpaka sasa imeshashushwa zaidi ya mara bilioni 5, ambayo ni namba kubwa sana katika magemu.
Rovio ina vituo 8 vya magemu duniani huku ikiwa na wafanyakazi 550 duniani kote. SEGA ikifanikisha umiliki wa kampuni hiyo basi kampuni itazidi kuwa kubwa.
Ningependa kusikia kutoka kwako, hebu niandikie hapo chini katika uwanja wa comment, je unaiona kampuni ya SEGA ikiendelea kukua zaidi ya hapa?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.