Ubisoft ni moja kati ya makampuni makubwa ya kuzalisha na kuendeleza michezo (magemu) mbalimbali ambayo makao yake makuu yapo ufaransa. Mara hii ikliwa na dhima ya kuongeza matawi mengi katika sehemu tofauti tofauti katika nchi za kigeni
Licha ya kuwa na tawi lake lingine nchini Singapore, kampuni kinasema kuwa liko katika mpango wa kuwa na offisi huko Manila katika nchi ya ufilipino. Ofisi hiyo itafungua milango kwa wafanyakazi wa nchi zingine katika sehemu tofauti tofauti duniani na kikubwa ni kwamba hata kwa wafilipino watapata ajira.
“ Kila siku Wafilipino wanatoka nje ya nchi yao kwenda kujitafutia furusa mbalimbali na nilikuwa mmoja kati ya hao watu miaka nane iliyopita na sasa nina furaha ya aina yake kurudi hapa kwa kishondo” – alisema mkurugenzi mpya wa Ubisoft wa Ufilipino
Kabla ya Ubisoft haijafungua tawi lake huko Manila, lilishangazwa kwa kuona limeajiri watu wengi sana katika matawi yake tofauti tofauti ambao walitokea nchini ufilipino. Baada ya kuona hivyo ndio wakaamua kabisa kwenda kufungua tawi huko huko. Hapa walitumia ujanja sana – wameenda kwenye samaki wengi – kwani wafanyakaze wake wengi wazuri walitokea nchi hiyo
Katika miaka mitano ijayo, kampuni la Ubisoft lina mpango wa kuongeza wafanyakazi wake kuyoka 50 mpaka kufikia 200. Ili kufanikisha hilo kampuni limeingia katika ushirikiano na chuo kikuu cha Manila, De La Salle katika kukuza watu maridadi katika njanja ya magemu ambao pia wanaweza wakabahatika kujipatia kazi katika kampuni la Ubisoft.
Kwa kufanya hivyo pia italisaidia kampuni katika kuajiri nguvu kazi ya kipato cha chini kwa kuwa nchi hiyo ina aina hiyo ya nguvu kazi (watatumia pesa ndogo kuwapata watu wenye uwezo wa juu)
Japokuwa ofisi bado haijafunguliwa rasmi lakini Ubisoft inasema imesahaanza ajiri watu na hata katika tovuti ya kampuni kuna nafasi mbalimbali za kazi zinatangazwa kwa ajili ya ofisi hiyo.