Game ya Mwanadada Kim Kardashian ‘Kim Kardashian; Hollywood’ ni Gemu ambalo linaruhusu wachezaji wake kuishi kama watu maarufu. Hili gemu ni la bure katika stoo zote za Android na iOs lakini wachezaji wanaweza tumia pesa ya ukweli katika kununua vitu ndani ya gemu mfano nguo na bidhaa nyingine. Hili swala limewafanya wazazi wengi kuona kwamba gemu hilo lina ‘link’ na kadi zao za benki wakati wakiwa wanangalia matumizi ya kadi zao yaliyofanyika kwa mda fulani (statement report). Makato hayo ambayo wanakwatwa bila kutegemea yamewekera sababu watoto wao ndio wanacheza sana gemu hiyo mpaka wanajikuta wanatumia taarifa za benki za wazazi wao ilimradi tuu kufurahia gemu hilo.
“Nafikiri mzazi inabidi uwe muwajibikaji, na usiache kadi yako ya benki sehemu ambayo mwanao anaweza kuchukua na kutumia kama anashida nayo” alisema Kim Kardashian
Kim K aligundua kua sio watoto tuu amabao wanatumia hela kwenye gemu hilo amesema hata mdogo wake wa kike wa miaka 17 Kylie Jenner alimpigia simu na kulalamika kuwa ametumia dola 300 za kimarekani kwenye gemu hiyo na anaomba ampatie ‘cheats’ ili aweze cheza kwa urahisi bila kunlipia chochote. Kim pia amesema hakuna kitu chochote kibaya kuhusiana na mazingira ya gemu hiyo ambayo yanamshawishi mtoto kutaka kuishi maisha ya kujulikana (superstardom) yaliyozungukwa na vitu vya thamani.
“Ndani ya gemu utagundua lina furaha na si la kulitilia maanani sana, ni gemu tuu, unachagua marafiki, unachagua nguo. Yaani ni gemu dogo tuu la kukuoa tabasamu kama vile unavyoona watu wakifurahia gemu la candy crush, Kwani ni kitu kizuri kupenda kula pipi? Hapana ila ni kitu watu wanapenda fanya. Magemu yote nafikiri yanaburudisha” alisema Kim.
Kim ameshangazwa na umaarufu wa game hiyo kwan ni kitu ambacho hakukitemea sio kwamba alilidharau bali anashukuru na kushangaa jinsi lilivyokuja kuwa. Kampuni nyuma ya gemu hilo Glu Mobile wamefurahishwa na gemu hilo
Je unafikiri hii Gemu ni sahihi kuchezwa na watoto, hawataharibikiwa? shusha mawazo yako sehmu ya comment
No Comment! Be the first one.