fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
simu Tanzania Teknolojia

Viettel, Kampuni Mpya ya Mawasiliano Tanzania

Viettel, Kampuni Mpya ya Mawasiliano Tanzania

Spread the love

viettel_tanzaniaMamlaka ya Mawasiliano, TCRA imeipa leseni ya mawasiliano ya simu ya mfumo wa 3G kampuni ya Viettel kutoka Vietnam. Juhudi za kampuni hiyo zilianza mapema mwanzoni mwa mwaka huu na tayari imeshaanza kufanya kazi katika nchi ya jirani, Msumbiji. Viettel inaingia katika wakati mgumu zaidi kiushindani katika biashara ya mawasiliano ya simu, ukitoa Vodacom, Airtel, Tigo, Zantel tayari pia kuna mtandao mwingine wa mawasiliano ulioingia hivi karibuni, Smart. 

SOMA PIA  Marufuku matumizi ya Bitcoin nchini Iran

Biashara ya Jeshi!

Viettel ni mtandao namba moja nchini Vietnam na unamilikiwa na jeshi la nchi hiyo. Kampuni hiyo imekuwa ikijitaidi kutafuta njia zingine za kukuza mapato yao kupitia kukuza huduma zao nje ya Vietnam.

Huduma yote katika mfumo wa 3G

Kampuni hiyo imehaidi kujenga mfumo wa mawasiliano nchi nzima katika 3G na sio 2G na EDGE. Hii itasaidia sana katika kufanya huduma yao ya intaneti kuwa ya uhakika zaidi kwani bado hadi leo baadhi ya mitandao mikubwa ya simu iliyopo inashindwa kutoa huduma ya uhakika ya 3G katika miji mikubwa tu nchini.

Ushindani Zaidi katika Biashara Hii inategemewa Watumiaji ndio Watakaonufaika Zaidi

Ushindani Zaidi katika Biashara Hii inategemewa Watumiaji ndio Watakaonufaika Zaidi

Pia wamehaidi kutoa huduma za intaneti ya broadibandi (broadband) katika mijini na katika miji midogo.

SOMA PIA  Instagram Wabadili Maamuzi!

Waziri Msaidizi wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Bwana January Makamba alisema ya kuwa wameitaka kampuni hiyo isambaze huduma ya fiba (Fibre) katika hospitali 150 za wilaya, ofisi 150 za serikali za wilaya, ofisi 65 za posta pamoja na shule 500 za sekondari. TTCL ipo wapi kufanya haya? Tuambie wazo lako katika hili.

SOMA PIA  ZIfahamu sifa zote za simu janja Xiaomi Mi 11

Kwa sasa kampuni hiyo baada ya kupata leseni hiyo inajikita katika kutengeneza mifumo yao vizuri na inategemewa wataanza kutoa huduma ifikapo Julai mwaka 2015.

Comrade Mokiwa

Mbunifu na mpenda teknolojia.

Muanzilishi wa Teknokona, TechMsaada na Teknokona Group LTD - WWW.TEKNOKONAGROUP.COM

Muda wangu umegawanyika kati ya kazi kibunifu @teknokonagroup na uandishi wa habari za Teknolojia hapa Teknokona Blog.

| mhariri(at)teknokona.co.tz |

Comment

Comments

  1. HAYA MAKAMPUNI YA SIM NAONA YANAENDESHWA KISIASA .MAANA WAMEPANDISHA BEI MAKSUDI KISHA WAMEPUNGUZA KASI UKIWAULIZA SABABU YA KASI NDOGO JIBU LAO UNATUMIA AINA GANI YA SIM .KILICHOBAKI SASA TUNASUBIRI WAGENI TUHAMIE HAWA WAMECHOSHA

Leave a Reply

Your email address will not be published.

TeknoKona Teknolojia Tanzania