Si mara nyingi unakutana na programu rahisi kutumia na ya kufurahisha kama BBC Swahili + VOA.
Programu hii Inatengenezwa na programa wa kisomali kwa lugha ya Kiswahili. BBC + VOA haina mbwembwe nyingi na inakuletea taarifa za habari moja kwa moja kutoka idhaa za kiswahili za BBC na VOA kwenye simu yako ya Android.
Kwa BBC, utapata kusikiliza pia Dira ya Dunia na Amka na BBC ulizozikosa siku, pamoja na vipindi vingine kama Michezo na wachezaji. Kwa upande wa VOA, utaweza kusikiliza Alfajiri, Jioni na Je, Nifanyaje moja-kwa-moja kutoka Washington.
Programu hii imeandikwa kwa kiswahili na inalenga watumiaji wa Kiswahili wanaopenda kupata habari za ukanda wa Afrika ya mashariki na kati kupitia simu zao. Ingawa ni ya kiswahili, programu hii bado ina vipande ambavyo havijatafsiriwa kwa kiswahili kama vile ilivyokuwa kwenye programu nyingi za mapokeo. Mpaka sasa, tunaweza kuhisi tu kwamba programa wa app hii ataendelea kuisuka na kuipa masasisho zaidi siku za karibuni lakini kwa sasa, shukrani kwake. Hakika tunaendelea kuweka lugha yetu mbele!
Kuishusha BBC + VOA kutoka playstore bofya hapa.
Unaonaje hadhi ya programu kama hizi zinazotumia lugha yetu ya Kiswahili? Je una programu nyingine mbadala kwa hii ambayo unayodhani ni nzuri zaidi? Tushirikishe.
No Comment! Be the first one.