Kodi za wananchi, makampuni, mashirika, n.k ndio zinazoendesha serikali kwenye nchi yoyote ili kuta maendeleo. Makampuni makubwa yanalipa kodi lakini inapobidi inabidi wapandishiwe kiwango.
Sauti ya wengi inaweza kuleta mapinduzi na hali ikabadilika kabisa. Wananchi wa Ufaransa wamekuwa wakiilalamikia serikali kutokana na mambo mbalimbali ambayo hayajawapendeza kitu ambacho kimesababisha maandamano makubwa na hata kushikiza rais wa nchi hiyo ajiuzulu.
Serikali imepata mbinu ya kuwatuliza wananchi wake na hii ni baada ya kutangaza kupandisha kodi iliyoanza kutumika Jan. 1 2019 kwa makampuni makubwa kama Facebook, Apple, Google, Amazon pamoja na mengineyo yanayojihusisha na teknolojia/utoaji wa huduma ya intaneti.
Ufaransa inatazamiwa kupata $572 milioni kutokana na kodi mbalimbali kwa makampuni makubwa pesa ambazo zitatumika kuhimarisha yale ambayo wananchi wameyapigia kelele.
Vyanzo: RT, QZ