Oppo ambao wanakuja kwa kasi kwenye suala zima la ushindani simu rununu ulimwenguni inatazamiwa kuishangaza dunia kwa toleo lijalo la simu janja inayofahamika kama Oppo Find X.
Sio mara moja tumeshawahi kuandika habari kuhusu bidhaa zinazotengenezwa na Oppo na kwa jinsi ambavyo zinapata soko zuri kuweza kushika nafasi za juu kushindana na makampuni nguli kama Apple na Samsung.
Kwa taarifa ambazo zipo zinaelezwa kuwa Oppo katika toleo lijalo la Find X huenda ikawa simu ya kwanza kuja na RAM ya GB 10.