Kujua kiasi cha kifurushi cha mtandao (internet data bundle) unachotumia ni jambo la msingi sana ukiwa unatumia computer, wengi tunatumia kompyuta (computer) kwenye maisha yetu ya kila siku ikiwa kazi nyingi pia hutegemea uwepo wa mtandao.
Kujua matumizi yako ya kifurushi cha mtandao kitarahisisha kupanga bajeti zako maana utajua ni kiasi gani kinatumika kwa siku na programu gani inatumia kiasi kikubwa cha kifurushi chako cha mtandao.
Namna ya kujua matumizi kifurushi cha mtandao (Internet data usage).
- Kwenye kompyuta yako bonfya Start kisha nenda kwenye Settings ya kompyuta, bofya kwenye Network & Internet, ukiwa kwenye hiyo sehemu “Network status” utaona kiasi cha kifurushi cha kimtandao (internet bundle) ulichotumia kwa mda flani, kama ni siku 30 itaoyesha.
- Ukibofya kwenye kwenye kifungo/button kimeandikwa “Data usage” utaona ni programu ipi inayoongoza kwa matumizi makubwa makubwa ya kifurushi ya mtandao na programu zingine zinazotumia kifurushi cha mtadao (internet data).
Jinsi ya kuweka kikomo cha matumizi ya kifurushi cha internet (Data limit).
- Bofya kwenye kifungo/button ya “Data usage” itakupeleka kwenye sehemu ya kuweka kikomo cha matumizi (Data limit), bofya kwenye sehemu imeandikwa “Enter limit” itakuonyesha kuweka machaguo yako, chagua kama ni mwezi n.k na pia weka kiasi ambacho unaona kikifikiwa iwe ni kikomo, mfano unaweza kusema kwa mwezi utumie 20GB ya kifurushi cha mtandao, hicho kiasi kikifikiwa hata kama ni ndani ya week, kompyuta yako haitoweza kuunganishwa na mtanadao mpaka ubadili mipangilio/Settings.
No Comment! Be the first one.