Soko la simu janja za kujikunja linazidi kutanuka kwa kiasi kikubwa, watengenezaji wengi wa simu janja wameingia katika soko hili. Honor nao wameamua kuja na Magic Vs ikiwa ni simu janja ya kujikunja.
Hii sio mara ya kwanza kwa kampuni ya Honor kutoka China kuja na simu ya kujikunja, na simu hii ni sehemu tuu ya maendelezo wa matoleo yake.
Uzito wa simu hii ni gramu 261 ambapo hii ni uzito kidogo ukilinganisha na simu nyingi za aina hii ambazo zipo sokoni.
Toleo hili linatumia chip kutoka katika kampuni ya Qualcomm ambayo ni Snapdragon 8+ Gen 1 na sifa yake nyingine ni kwamba simu hii inajikunja bila ya kuacha nafasi.
Simu hii inakuja katika 12/256 GB na 12/512 GB katika ujazo wake wa uhifadhi na RAM. Simu hii inakuja na peni ambayo inajulikana kama Magic Pen ambayo itakua inatumika baada ya kuunganisha na Bluetooth.
Ikiwa imekunjuliwa kioo chake cha OLED kina inchi 7.9 kikiwa kimeambatana na 2272×1984 pixels.
Ikiwa imekunjwa kioo cheke cha OLED kina inchi 6.45 na kinakuwa kimeambatana na 2560×1080 pexels
Kwa maajribio ambayo yamefanyika na Honor wenyewe wanadai kwamba simu hiuo inaweza kustahimili mikunjo zaidi ya 400,000 hii kwa haraka haraka ni zaidi ya miaka 10 ya matumizi.
Simu hizi zitaanza kupatikana rasmi katika masoko ifikapo novemba 30, huku baadhi ya watu wataanza kupata bidhaa hii kama wakitoa oda zao kabla ya simu kufika sokoni huko nchini china
Ukaichana na soko la China kampuni bado haikuweka wazi juu ya soko la dunia nzima litakavyokua lakini vyanzo mbalimbali vinasema kuwa itaanza kupatikana kote ndani ya robo ya kwanza ya mwaka 2023.
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika eneo la comment, je ushawahi kutumia simu ya kujikunja? Au simu kutoka katika kampuni ya honor? Niambie uzoefu wako, hebu tutete kidigo..!
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.