Kufuatia uzinduzi wa simu za iPhone kwa mwaka 2018 ambazo zinahusisha iPhone XS, iPhone XS Max na iPhone XR, imebainika kwamba sasa simu zake nyingi za modeli zilizopita, ikiwamo iPhone X, sasa hazitatengezwa tena.
Simu hizo zilizoondolewa sokoni, na ambazo pia zimefutwa rasmi katika tovuti ya Apple ni pamoja na iPhone 6S na iPhone SE, hiyo ikimaanisha kuwa sasa huwezi tena kununua iPhone yenye sehemu ya kuchomeka spika za masikioni ukubwa wa milimita 3.5.
Habari njema kwa mashabiki ni kwamba, Apple bado inauza iPhone 7, iPhone 8 na iPhone 8 Plus katika tovuti yake hivyo kuwa bidhaa pekee za iOS unazoweza kuzinunua moja kwa moja kutoka kwao.