Honor ni chapa ambayo mara ya kwanza kabisa ilikua inamilikiwa na kampuni ya Huawei na baadae ukauzwa na ikawa inajitegemea, kwa sasa chapa hiyo inakuja na program endeshi ya kwake inayojulikana kama MagicOS 7.0.
Honor ni chapa ambayo inazalisha mambo/vitu vingi sana vinavyohusiana na mambo ya teknolojia kama vile simu, kompyuta, programu endeshi (MagicOS 7.0 n.k.
Kampuni hii makao makuu yake ni china, na kwa sasa imekuja na programu endeshi ambayo inaitwa MagicOS 7.0.
Kingine kizuri kuhusiana na programu endeshi hii inadhaniwa kuwa inaweza kuendana kabisa na HarmonyOS –ya Huawei—na hata iOS –ya Apple—hapo baadae.
magicOS 7.0 inakua inahusisha teknolojia ya MagicRing, Magic Live, Turbo X na MagicGuard ambazo kwa namna moja au nyingine zitakua na uwezo wa kutambua chip tofauti tofauti na hata programu endeshi zingine.
Mkuu wa Hanor, Bwana George Zhao amesema kwamba ana Imani kubwa sana na programu endehsi hii na ina mrahisishia sana mtumiaji katika matumizi ya kifaa chake.
Ikumbukwe Honor ilaichana kabisa na Huawei mwezi novemba 2020 na licha ya kujitegemea kampuni imekua bado ikifanya vizuri sana.
Kwa robo ya tatu ya mwaka 2022 chapa ya Hanor iliweza kusafirisha na kuuza simu milioni 12.7 ndani ya nchi ya China tuu.
Kwa Vifaa Vya Honor, MagicOS 7.0 itaanza kupatikana kwa vifaa vifuatavyo na muda wake:
December 2022
- Honor Magic V
- Honor Magic3 Ultimate Edition
- Honor Magic3 Pro
- Honor Magic3
- Honor V40
January 2023
- Honor Magic4 Supreme Edition
- Honor Magic4 Pro
- Honor Magic4
February 2023
- Honor 70 Pro+
- Honor 70 Pro
- Honor 70
March 2023
- Honor 60 Pro
- Honor 60
- Honor 50 Pro
- Honor 50
April 2023
- Honor X40 GT
May 2023
- Honor V40 Light Luxury Edition
- Honor X40
- Honor X30
Ningependa kusikia kutoka kwako, naindikie hapo chini katika eneo la comment, je hii umeipokeaje, je unadhani programu endeshi hii itakua na ushindano mkubwa kwa programu endeshi ambazo bado zipo sokoni?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.