Wachoma moto minara ya 5G kwa hofu ya kwamba 5G inasambaza Coronavirus
Nchini Uingereza watu kadhaa wachoma moto minara ya 5G na vifaa vyake kutokana na kuamini habari za uongo kwamba teknolojia hiyo inasambaza virusi vya Corona.
Nchini Uingereza watu kadhaa wachoma moto minara ya 5G na vifaa vyake kutokana na kuamini habari za uongo kwamba teknolojia hiyo inasambaza virusi vya Corona.
Baada ya utafiti wa muda mrefu matokeo ya majaribio ya wanasayansi nchini Italia yanaonesha kuna uwezekano mkubwa wa kuwa na chanjo ya UKIMWI (Upungufu wa Kinga Mwilini) katika miaka ya hivi karibuni.
Kitengo cha teknolojia na sayansi za kimaisha cha ALPHABET (kampuni mama ya Google), kipo katika hatua za mwisho kuja na viatu vyenye uwezo wa kumpima mvaaji uzito..
Kampuni kubwa ya soda duniani, Coca Cola, wameweka dola milioni 1 za Kimarekani (zaidi ya Tsh bilioni 2) kwa ajili ya shindano la kuja na sukari mbadala ya kutumika kwenye soda zake.
Watafiti nchini Marekani wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa katika majaribio ya njia mpya na ya kwanza kwa wanawake kuweza kujikinga dhidi ya maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi na sasa utafiti huo kuamia barani Afrika.
Watoto watano wamefanyiwa upasuaji na kuwekewa vifaa maalum vya kusaidia kusikia (Cochlear Implant) jana wamewashiwa vifaa hivyo ili waweze kusikia kwa mara ya kwanza.
Moja kati ya magonjwa ambayo ni tishio kwa binadamu basi saratani ni mojawapo na kibaya zaidi linaenea mwilini kwa haraka sana bila kusahau matibabu yake si nafuu.
Sayansi ya uzazi inazidi kuwa na mapya kila leo jambo linalopelekea kuleta matumaini katika utatuzi wa changamoto mbalimbali ambazo sekta ya afya na sayansi ya uzazi inakumbananazo.
Mahakama moja nchini Italia imetoa hukumu kwa mfanyakazi wa kampuni ya Telecom Italia kulipwa fidia kwa kupatwa na uvimbe katika ubongo uliosababishwa na matumizi ya muda mrefu ya simu ya mkononi.
Binti wa miaka 25 amefariki baada ya upasuaji wa kuongeza makalio kwenda ndivyo sivyo, kwa mujibu wa polisi Ranika Hall kutoka Missouri Marekani amekumbwa na umauti katika kliniki ya mambo ya urembo mjini Miami ambako alikuwa anafanyiwa upasuaji.
Timu ya madaktari wamefanikiwa kufanya upasuaji na kuutoa mkasi ndani ya tumbo la mwanaume mmoja huko Vietinamu, mkasi huo ambao ulisahauliwa katika upasuaji mwingine aliofanyiwa mgonjwa huyo miaka 18 iliyopita.
Oktoba na Novemba na mfululizo wa miezi ya uamko wa elimu ya saratani. Kampuni ya Microsoft imetangaza miradi kadhaa wanayolenga kufanya ili kusaidia mapigano dhidi ya magonjwa ya saratani (Cancer). Miradi hii itatumia teknolojia za kufundisha kompyuta.
Wiki chache zilizopita, washika dau mbalimbali wa sekta ya Afya, pamoja na Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto walifanya uzinduzi wa tovuti maalumu kwa ajili ya taarifa kuhusu afya ya figo, uzinduzi uliofanyika mjini Dar es Salaam.
Tumezoea kuona teknolojia ya 3D katika magemu au tukienda kuangalia sinema au hata majumbani kwetu kwa wale wenye Tv’s ambazo zina teknolojia ya 3D watakuwa si wageni kwa hili lakini teknolojia hiyo inaonekana kwenda mbali zaidi.
Kwa mara ya kwanza duniani roboti imetumika kumfanyia upasuaji wa macho mgojwa. Upasuaji huo ulifanyika kwa mafanikio na huwenda katika siku za usoni roboti wakatumika kwa wingi kumfanyia mtu upasuaji.
Mwanamke ambaye anataka kutumia mayai ya uzazi ya bintinye ili kumzaa mjukuu wake ameshinda kesi mahakamani na kuruhusiwa kufanya hivyo.
Wanasayansi katika Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine nchini Tanzania wanapanga kuwatuma panya waliopokea mafunzo kwenda kutumiwa kugundua kifua kikuu nchi za nje.
Kampuni moja ya madawa imepata kibali cha kufanya majaribio ya chanjo ya Virusi vya Zika kwa binadamu, majaribio haya ni ya kwanza na yanalenga kuona jinsi ambavyo dawa hii inapokelewa na miili ya binadamu.
Hivi karibuni hospitali mbili nchini Ubeligiji zimeamua kutumia roboti kufanya kazi ambazo binadamu angeweza kuzifanya.
Upo hapo? Mswaki wa dola 400 za kimarekani utakaokusafisha wakati huo huo ukiwa unakupa video za moja kwa moja (LIVE) za kinywani mwako kupitia simu yako.