fbpx
Afya, Microsoft, Teknolojia

Microsoft Kutumia Utashi wa Kompyuta (AI) kutatua Saratani

microsoft-kutumia-utashi-wa-kompyuta-kutatua-saratani

Notice: Trying to access array offset on value of type null in /home/teknoloj/public_html/wp-content/plugins/intelly-related-posts/includes/core.php on line 163
Sambaza

Oktoba na Novemba na mfululizo wa miezi ya uamko wa elimu ya saratani. Kampuni ya Microsoft imetangaza miradi kadhaa wanayolenga kufanya ili kusaidia mapigano dhidi ya magonjwa ya saratani (Cancer). Miradi hii itatumia teknolojia za kufundisha kompyuta.

Mfano kwa kupitia mradi walioupa jina la Hanover, Microsoft wanatazamia kutoa maelezo-tiba yanayomlenga mtu kipekee na kwa uhakika wa hali ya juu kwa kila mgonjwa wa saratani kwa kuwasaidia wataalamu wa magonjwa hayo kwa kupitia maelfu ya stadi za magonjwa hayo kwa muda mfupi.

INAYOHUSIANA  Apple Kuja Na Emoji Mpya Katika Vifaa Vya iOs na macOS!

Kwa maelezo ya Microsoft, wataalamu wa Project Hanover wanatumia taarifa maalumu za serikali ya Marekani kutengeneza teknolojia ya kufundisha kompyuta kupitia mamilioni ya machapisho ya kitaalamu bila kutegemea mtu na kuziweka kwenye mpangilio maalumu wa data (structured database).

Katika upande mwingine wa stadi za saratani, Microsoft wanawasaidia wataalamu wa mionzi hosipitalini kufuatila mwenendo wa ugonjwa huo.

Wakati wataalamu hao wananweza kwa haraka kutazama vipimo vya CT-scan kutambua kama mtu ana uvimbe (tumor), jicho la binadamu haliwezi kutambua mabadiliko ya seli.

INAYOHUSIANA  Clickfarms: Wauza Likes, Shares, na Comments wakamatwa nchini Thailand

Microsoft wametangaza teknolojia nyingine ya kuchunguza nini kinachotokea kwenye seli punde ugonjwa wa saratani unapotokea. Teknolojia hii itasaidia kutambua saratani mapema zaidi na kutabiri jinsi mgonjwa atajisikia baada ya kupewa dawa tofauti.

Kwa kuhitimisha, Microsoft wamesema kwamba wanatumia watafiti wao kujaribu ku-elekeza (ku-program) seli za binadamu badala ya kompyuta. Ingawa wanasema kwamba wako mbali na kufanikisha hili jambo, kiufundi linawezekana kabisa. Kwa sasa wanachofanyia kazi na kuweza kuelewa seli kwa undani zaidi kama wanavyoielewa kompyuta.

INAYOHUSIANA  Simu Yako Haiwezi Kukupa Saratani

Microsoft siyo kampuni kubwa pekee inayojihusisha na kutumia rasiliamali zake kupigana na saratani. Kampuni ya Google (ama Alphabet) nayo ina mipango mikubwa ya mapigano dhidi ya magonjwa ya saratani kupitia mradi wake wa kusaidia madaktari kufanya maaumzi.

Kumbuka kusambaza makala na pia kuungana nasi kupitia Facebook, Twitter, Instagram, YouTubeTelegram na Google Plus

Chanzo: zdnet.com

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Notice: Trying to access array offset on value of type null in /home/teknoloj/public_html/wp-content/plugins/intelly-related-posts/includes/core.php on line 163

ecay

Ninafuatilia teknolojia kila siku na ninapenda kutoa ujuzi wangu kuhusu teknolojia. Karibu tuzungumze kuhusu teknolojia hapa teknokona!