Kitengo cha teknolojia na sayansi za kimaisha cha ALPHABET (kampuni mama ya Google), kipo katika hatua za mwisho kuja na viatu vyenye uwezo wa kumpima mvaaji uzito..
Ripoti iliyotolewa na chombo cha habari cha CNBC inasema wamefikia pazuri sana kwa sasa kwani wanatafuta kampuni ya kushirikiana nayo katika utengenezaji wa viatu hivyo.
Ni kawaida sana kwa makampuni chini ya ALPHABET -hii ikiwa ni pamoja na Google, kuwa na mfumo wa kiutafiti na utengenezaji wa apps au programu endeshaji na kisha kutafuta mshirika (partner) mwenye kiwanda ili kutengeneza bidhaa husika.
Hatua hii inaonekana ni juhudi ya Alphabet kudhidi kujizatiti katika teknolojia zinazohusiana na ufuatiliaji wa hali ya afya kwa watumiaji wake.
Verily kitengo cha sayansi ya maisha, ndio wanakuletea teknolojia ya viatu vyenye uwezo wa kumpima mvaaji uzito wake na kuendelea kurekodi data hizo
Biashara ya vifaa vya teknolojia kwa ajili ya ufuatiliaji na ushahuri wa kiafya imekua kwa kasi katika miaka ya hivi karibuni. Hii inajumuhisha uwezo wa saa janja zinazofuatilia mambo kama hatua za utembeaji, kiasi cha ulalaji n.k.
Programu endeshaji ya Google kwa ajili ya vifaa vya mazoezi inayoenda kwa jina la Google’s Wear OS ndio programu inayotumika zaidi kwenye vifaa hivi.
Soko la bidhaa hizi linategemewa kufikia mauzo ya dola bilioni 25 mwaka huu 2019..na hadi kufikia zaidi ya dola bilioni 27 ifikapo mwaka 2022 kulingana na Forbes.
Inategemewa viatu hivi vyenye uwezo wa hadi kuwasiliana na app za afya kwenye simu janja vitaweza kuingia sokoni ndani ya muda wa miaka miwili kuanzia sasa.
Wezesha bando kwa kutuma kiasi chochote kupitia Selcom, kwenye simu yako bofya *150*50*1# kwenye namba ya malipo weka 60751369 jina litakuja TEKNOKONA.
Mbunifu na mpenda teknolojia.
Muanzilishi wa Teknokona, TechMsaada na Teknokona Group LTD - WWW.TEKNOKONAGROUP.COM
Muda wangu umegawanyika kati ya kazi kibunifu @teknokonagroup na uandishi wa habari za Teknolojia hapa Teknokona Blog.
| mhariri(at)teknokona.co.tz |