Mpira wa miguu ni mchezo uliotawala Afrika na watu wanapenda kutabiri na kubashiri mechi za mpira. Kubashiri kunategemea na mtu mwenyewe kuona kama kubashiri mpira ni sawa au kitu kibaya. Kwa wanaopenda kutabiri, kwa sababu binafsi na kiutani, Goal.com Live Scores ni programu ya simu, tableti na kompyuta inayotoa taarifa mbalimbali kusaidia kutabiri mechi za mpira wa miguu.
Shusha na pakia app ya Goal Live Scores kwenye android, windows au iOS au kufungua tovuti ya goal.com/livescores. Ukifungua utakutana na matokeo ya mechi zlizopangwa kuchezwa kwa siku tofauti. Kwenye app za simu na tableti, utakaribishwa na huduma ya kuchagua timu na mashindano unayopendelea zaidi. Ukimalizana na hilo, utakuwa tayari kutumia kifaa chako kipya kwa utabiri kwa kuchunguza magoli, maoni ya washabiki wengine, takwimu, ‘form’ na mengineyo.
Chagua Mechi unazotaka kufuatilia
Ukiingia tu kwenye Goal Live utapata muonekano mrahisi wa mwanzo ambao juu yake una tarehe ambazo unaweza kuona mechi zote zinazoendelea, zinazokuja na zilizopita. Hii inakupa urahisi wa kufuatilia utabiri wako. Weka nyota kwa mechi unayotaka kuifuatilia ili kuiweka juu kabisa kwenye orodha ya mechi za siku.
Chunguza Muda Magoli yalipofungwa
Ukiangalia kwenye kipengele cha ‘Details’ utaweza kuona taarifa kwa ufupi za magoli na kadi. Muda wa kufungwa magoli na wafungaji zinatumika na watu kuchambua timu na kutabiri kama wana mtindo wa kufunga ndani ya kipindi cha kwanza au la. Pamoja na hayo, hiki kipengele kinakupa mazingira ya mechi inayochezwa au kuchezwa, yani, uwanja, refa na makocha.
Angalia Kura za Maoni kutoka Mashabiki wengine
Chini kabisa kwenye kipengele cha ‘Details’ utaona sehemu ya ‘Predict’ ambayo inaonyesha kura za maoni zilizokusanywa na Goal kutoka kwa mashabiki. Hautaweza kuona kura hizi kama wewe mwenyewe haujatupia kura yako, isipokuwa kama mechi ilishachezwa, utaziona bila kupiga kura. Kuona kura napo kunasaidia kufanya maamuzi ila, haihitaji akili nyingi kujua kwamba hizi ni kura za kishabiki, hazina ukweli mwingi na inategemea wingi wa mashabiki wa timu husika. Tumia hii kwa timu ambazo hujui kujua wingi wa mashabiki wake, ambacho kitakusaidia kujua nguvu yake popote ilipo duniani.
Chunguza Mechi kwa Undani
Ukichagua mechi yoyote iliyopita kwenye Goal Live, na kuangalia kipengele cha ‘Stats’ utaona taarifa za mechi nzima, kuanzia madhambi, umiliki wa mpira, mashuti, miamba hadi ‘offside’ zinazoonesha timu ipi iliipiku nyingine, kitu ambacho kitakusaidia sana kujua zaidi kuhusu timu ambayo pengine huijui vizuri au una mashaka nayo.
Chunguza Mwenedo (‘Form’) ya Timu husika
Ukisogea kwenye kipengele cha ‘Form’ kwenye kwenye mechi unayotaka, utaona orodha ya mechi kwa timu zote mbili inayokuonesha mwenendo (‘form’) ya timu hizo kwa mechi tano zilizopita ambazo unaweza kuzichambua kiundani ukitaka. Goal Live inakupa urahisi kwa kutofautisha matokeo ya suluhu, ushindi na kushindwa kwa rangi za njano, kijani na nyekundu kukuokolea muda. Pia mwishoni utaweza kupata pia orodha ya mechi zilizopita ambazo timu hizo zilikutana.
Angalia Msimamo wa Ligi au Kundi kwa mechi husika
Msimamo wa ligi au kundi nao unasadia sana kuonesha ushindani kati ya timu mbili na umuhimu wa mechi unayofuatilia. Ukitafuta mbele kwenye kipengele cha mwisho cha ‘Table’ utaweza kuona msimamo wa mashindano ya mechi hiyo.
Fuatilia Mechi zinazoendelea Muda Huo Huo (‘Live’)
Ukimaliza kuchambua mechi unazotaka, Goal Live ina sehemu ya kuangalia mechi za papo kwa hapo. Kwa wale ambao wamemaliza kuangalia mechi zinzowahusu na wanataka kuangalia mechi
zinazoendelea muda wowote, sehemu yoyote duniani, basi wanaweza kutumia
chaguzo hii kujinufaisha na matokeo safi ya laivu.
Pata Pointi za Ubashiri (‘Odds’) za Mechi
Hii ni kwa wale watakaotaka zaidi ya utabiri binafsi na wa utani. Goal Live inakupa ‘Odds’ kwa mechi tofauti zinazokuja ukiingia kwenye kurasa yao ya livesores kwenye tovuti na kuchagua ‘Show Odds’ pale juu kulia ya My Scores.
Goal Live Scores wamefanya utabiri kuwa wa makini na kitu kirahisi kutokana na wingi wa chaguzo walizokuwekea kwenye programu hii ndogo, isiyotumia chaji nyingi, wala kiasi kikubwa cha intaneti. Live ni rahisi kuitumia na ni programu nzuri sana kwa mfuatiliaji yeyote wa mpira wa mguu duniani kwa kuwa inafuatilia karibu ligi zote maarufu na hata Ligi kuu Bara ya hapa nyumbani, Tanzania.
Mambo Mengine ya Kufurahisha
-> Tafuta timu yoyote na uifuatile.
-> Fuatila Ligi na kombe lolote duniani!
-> Goal Live inakupa matokeo ya haraka zaidi kuliko programu nyingine za mpira wa miguu
-> Angalia match-cast kukonyesha jinsi mechi inavyoenda, sekunde baada ya
sekunde.
-> Badilisha mishtuo ya taarifa wakati wowote.
Mambo ambayo Pengine Hayafurahishi.
Programu hii kwa sasa haina ‘Sign-in,’ kwa hiyo, hautaweza kuhamisha mapendekezo ya timu na mipngilio yako kwenye simu nyingine. Kuipangila Goal Live kwenye simu nyingine, itakulazimu uanze upya kuipangila.
Picha Na:
No Comment! Be the first one.