Mwezi wa nane tuliandika kuhusu huduma ya intaneti ya bure kwa wakazi wa Zambia – Zambia yapata Internet ya Bure inayotokana na juhudi za kampuni ya Facebook na wiki hii huduma hiyo imekuja pia Tanzania kupitia ushirikiano na kampuni ya simu ya Tigo. Bwana Mark Zuckerberg alitangaza rasmi kupitia akaunti yake ya Facebook na pia kampuni ya Tigo imefanya utambulisho rasmi.
Je internet.org ni nini?
Internet.org ni harakati iliyoanzishwa na mwanzilishi wa Facebook, Bwana Mark Zuckerberg mwaka 2013 ni mkakati wa kuleta huduma ya intaneti kwa watu wengi zaidi, katika ubora na kutokuwa ghari. Kwa sasa katika kufanikisha hili Facebook imepata waunga mkono kama vile Samsung, Ericsson, MediaTek, Nokia, Opera na kampuni ya Qualcomm.
Kwa ufupi lengo kuu ni kutengeneza kitu kama 911 cha intaneti, yaani huduma ya bure ya intaneti kuwawezesha watu kutumia huduma kadhaa muhimu bure.
Baada ya mafanikio ya nchini Zambia, Facebook wameweza kuleta huduma hiyo Tanzania kupitia ushirikiano na kampuni ya simu ya Tigo.
Kwa sasa huduma utakazoweza kuzipata bure ndani ya mfumo wa internet.org ni zifuatazo;
- AccuWeather – Hali ya hewa
- BabyCenter & MAMA – Matunzo ya watoto
- BBC News & BBC Swahili – Habari za kitaifa na kimataifa
- BrighterMonday – Nafasi za Ajira
- The Citizen – Gazeti
- Facebook – Mtandao wa Kijamii
- Facts for Life – Taarifa za Afya kutoka UNICEF
- Girl Effect – Afya za Wanawake wadogo na taarifa dhidi ya umasikini
- Messenger – App ya kuchati ya Facebook
- Mwananchi – Gazeti
- Mwanaspoti – Gazeti la michezo
- OLX – Matangazo
- Shule Direct –Elimu Mtandaoni
- SuperSport – Habari za michezo
- Tanzania Today – Habari
- Wikipedia – encyclopedia
Huduma ya internet.org unaweza ipata kupitia simu janja za Android kwa kubofya HAPA – Google PLay, pia unaweza kuzipata kwa kutembelea moja kwa moja mtandao wa www.internet.org kupitia simu yako, njia nyingine ni kupitia Opera Mini.
No Comment! Be the first one.